HISTORIA YA WILLIAM B MKAPA



 Huyu ndie William mkapa,

Alizaliwa 1938,ana watoto 2,

anashutumiwa kwa kauli tata na ufisadi.

Na Mariam Michael.

Mkapa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere. Na Chuo Kikuu cha Columbia Nafasi alizoshikilia zamani ni pamoja na kuwa afisa wa utawala huko Dodoma na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu.

Yeye pia aliongoza ujumbe wa Tanzania huko Marekani na alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kutoka 1977 hadi 1980 na kutoka 1984 hadi 1990.

Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kwa kumuunga mkono kwa nguvu rais wa zamani Julius Nyerere
WWW.HAKILEO.BLOGSPOT.COM

Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi,Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005.

Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha makampuni yanayomilikiwa na serikali na akaweka sera za soko huru.

Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.

Amekashifiwa kwa upungufu wa baadhi ya jitihada zake za kupambana na ufisadi vilevile njia yake duni ya kutumia fedha. Alitumia £15 milioni kununua ndege ya kibinafsi ya kirais, vilevile karibu £30 milioni kwa vifaa vya angani vya kijeshi ambavyo wataalam waliona yalizidi mahitaji machache ya majeshi ya nchi .

Ilikuwa juu ya ununuzi huu wa mwisho ndipo Katibu wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza wa wakati huo Clare Short alielezea hasira ya umma, na kusababisha yeye kujulikana kama 'Mama Radar' katika vyombo vya habari vya Tanzania.

Baada ya kutoka ofisini kutokana na kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa, Mkapa anakumbwa na shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa nishati na madini Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" yenye faida kubwa katika Nyanda za juu za kusini mwa Tanzania bila taratibu zifuatazo.

Kwa kujibinafsishia mwenyewe mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, alivunja katiba ya Tanzania ambayo haimruhusu rais kufanya biashara yoyote katika ikulu.

Aliteuliwa katika Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Aga Khan mwezi Novemba 2007.

Mkapa aliitawala Tanzania kwanzia mwaka 1995mwezi wa kumi tarehe 23 hadi 21/12/2005 ambapo alimwachia raisi aliemtangulia ambae ni Jakaya Kikwete, na aliemtangulia ni raisi Ali Hassan Mwinyi maarufu kama Ruksa.

Makamo wake wa raisi wa kwanza ni Omar Ali Juma (1995–2001) na alipokelewa na Ali Mohamed Shein (2001-05) ambae hivi sasa ni raisi wa Zanzibar na chama chake cha kisiasani CCM.

Mbali na hayo aliwahi pia kuwa waziri wa habari na utangazaji mwaka 1990 – 1992.Mkapa alizaliwa 11/ 1938 kwa hiyo hivi sasa ana umri wa miaka 75. Eneo alililo zaliwa ni Ndanda, Masasi, hapa Tanzania.



Mh.Mkapa amemuoa binti wa kabila la kichaga aitwae Anna Mkapa na amefanikiwa kupata watoto wawili.

Kwa upande wa fani mkapa ni mwandishi wahabari na mwanadiplomasia.
Licha ya wasifu wake pia Benjamin William Mkapa, anazo sifa zake. Inasemekana ni rais aliyekuwa na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha juu ya jambo lolote lililoelekezwa kwake likihitaji ufafanuzi.

Wapo wanaosema kwamba hiyo inachangiwa na uwezo wa kiakili alio nao rais huyo mstaafu, lakini wengine wanasema hicho ni kipaji cha mtu wala hakina uhusiano na uwezo wa kiakili.

Lakini hata hivyo baadhi ya watu aliosoma na Mkapa katika sehemu mbalimbali, kuanzia shule za chini, shule za kati, St. Francis Pugu na hata Chuo Kikuu Makerere, wanasema Mkapa alikuwa na uwezo mkubwa darasani, vilevile uwezo mzuri wa kujieleza na kuitetea hoja yake hasa wakati wa midahalo.
HUYU NDIE MKEWE  Wanasema ni uwezo huo uliomfanya arushwe madarasa. Inasemekana sekondari aliisoma kwa miaka mitatu badala ya minne, na wengine wanasema kwamba shahada nayo aliisoma kwa miaka miwili badala ya mitatu, kama si kutia chumvi.

Pengine ni ukweli huo uliomshawishi Baba wa Taifa, ambaye kipindi fulani alikuwa mwalimu wake Mkapa, amwekee kifua ili aweze kuupata urais wa Tanzania. Mwalimu alikuwa anaonyesha bila kificho jinsi alivyomuamini Mkapa. Na alikuwa anaonyesha uhakika kwamba Mkapa angeweza.

Pamoja na Mkapa kuonekana hivyo kwa Mwalimu likaja kujitokeza tatizo ambalo nahisi hata Mwalimu hakulijua. Tatizo la kujiona yeye anajua, lakini waliobaki wote ni majuha, hawaelewi kitu. Mkapa akaanza kutumia usemi wake maarufu wa kwamba watu ni wavivu wa kufikiri. Akawa anaamini kwamba watu hawafikiri kabisa.

Kwa kuamini hivyo, kwamba wananchi hawafikiri, Mkapa akasema bila haya kwamba Ilani ya chama chake kiliyoitumia kumweka madarakani ilikuwa haitekelezeki. Alisema hivyo bila kujali kama wananchi wanajiuliza aliwezaje kukinadi kitu kisichotekelezeka.

Baada ya kubanwabanwa kuhusu kauli hiyo akasema nakanusha, sikusema hivyo! Si aliamini kwamba wananchi hawafikiri!

Mambo aliyoyafanya Mkapa kudhihirisha kwamba Watanzania ni wavivu wa kufikiri akiwa madarakani ni pamoja na kuuza au kubinafsisha mashirika ya umma na kutopenda kusikia kitu kikiitwa cha umma (kama tulivyo kwisha kuona hapo awali). Nadhani angekuwa na uwezo hata neno umma angelifuta kwenye msamiati wa Kiswahili.

Akauza nyumba za serikali kana kwamba utawala wake ulikuwa wa mwisho na baada ya hapo kusingekuwepo na serikali nyingine ambayo watumishi wake wangehitaji mahali pa kuishi. Yeyote aliyekwenda kinyume na mtazamo wake alionekana ni mvivu wa kufikiri. Mwisho wa yote akaamua kusajili kampuni ya biashara akitumia anwani ya Ikulu, Ikulu ikageuka sehemu ya biashara.

Na wakati anamaliza muda wake, wa kuwa madarakani kwa mujibu wa sheria, akaondoka kimyakimya bila kuwaeleza wananchi alichokivuna akiwa Ikulu. Hakutaka wananchi wakielewe kilichotokana na biashara yake aliyoifanya akiwa Ikulu.

Akasahau kwamba ni yeye aliyetutajia mali zake wakati anaingia Ikulu. Ni lazima hiyo yote ilichangiwa na imani yake ya kwamba wananchi ni wavivu wa kufikiri.

Iwapo Mkapa angeelewa kwamba wananchi wanaweza kufikiri japo kidogo asingediriki kufanya biashara akiwa Ikulu kinyume na kampeni iliyomwingiza pale.

Kampeni hiyo ni ile iliyosimamiwa na Baba wa Taifa ya kwamba Ikulu hapauzwi nyanya, Ikulu si pango la walanguzi, Ikulu ni sehemu takatifu. Utakatifu huo wa Ikulu Mkapa akaupoteza.

Baada ya Mkapa kutoka madarakani wadau wakahoji ni kwa nini asiulizwe sababu za kuinajisi Ikulu yetu, lakini aliyempokea kijiti, JK, akasema hapana, tumuache mzee apumzike kwa utulivu.

Wananchi wakanyamaza wakidhani Mkapa anapumzika kweli.

Lakini sasa tunamuona tena Mkapa majukwaani akiyanadi mazuri yake bila kuyagusia yale tuliyoambiwa tuyaache, ili akapumzike kwa utulivu.

Lakini kwa vile kaamua kujileta mwenyewe tena ulingoni tukimuunganishia hapo yale maswali yetu tutakuwa tumemkosea adabu?

Maana inasemwa kwamba mdogo amheshimu mkubwa, lakini ili heshima hiyo iwe na maana inabidi mkubwa ajiheshimu kwanza kwa kutambua uwepo wa mdogo.

Iwapo mtu mzima atavua nguo mbele ya watoto na kubaki uchi haitawazuia watoto kusema kwamba mzee fulani kakaa uchi na hata kumcheka wakati mwingine.

Si kwamba watoto wanakuwa wamemkosea adabu, ila mwenye kukosa adabu ni yeye mwenyewe anayekosa kutambua uwepo wa watoto kabla ya kufanya uhayawani wake.

Sasa Mkapa yamemkuta, imani yake ya kwamba Watanzania ni wavivu wa kufikiri imemtuma apande jukwaani Arumeru Mashariki kwa kisingizio cha kumnadi mgombea wa CCM kumbe anatafuta nafasi ya kujitakasa mwenyewe.

Badala ya kumnadi mgombea wa chama chake kuonyesha uwezo alio nao wa kuwawakilisha wana Arumeru, Mkapa akaanza kujinadi yeye mwenyewe na akionyesha uwezo alionao yeye kana kwamba yeye ndiye anayetakiwa kuchaguliwa kuwawakilisha wana Arumeru!

Mkapa akaeleza atakavyoyashughulikia matatizo ya Arumeru, hususan tatizo sugu la ardhi, kwamba atalibeba tatizo hilo na kwenda nalo mpaka kwa Rais Kikwete na kumshauri alishughulikie kwa kipaumbele cha kwanza.

Baada ya hilo Mkapa akateleza na kuanza kumshambulia Naibu Meneja wa Kampeni wa CHADEMA, Vincent Nyerere, Mbunge wa Musoma Mjini, kwamba si mtoto wa Nyerere.

Kwa msisitizo Mkapa akasema hamtambui Vincent katika familia ya Nyerere. Kwa maneno mengine alionyesha kwamba Vincent ni tapeli kwa kutumia jina la Nyerere.

Nianze kuliangalia hili la kwanza la kuyashughulikia matatizo ya ardhi ya Arumeru badala ya matatizo hayo kushughulikiwa na mgombea aliyekuwa anamnadi.

Matatizo ya ardhi katika Arumeru si ya jana wala juzi, hayakuanza kujitokeza baada ya Mkapa kustaafu urais. Kwa hiyo katika hili Mkapa alionesha udhaifu mkubwa sio wakati akiwa raisi tuu kwa kuto lishuhulikia bali hata wakati wa kampeni

Mpaka hapo aliendelea kudhiirisha ya kwamba anaamini wananchi wanatatizo la kufikiria.

Sasa tuangalie jinsi Mkapa alivyoteleza na kuangukia kwenye familia ya Baba wa Taifa. Anadai kwamba Vincent si mtoto wa Nyerere! Lakini wakati akionyesha uhakika wake huo kashindwa kueleza kijana huyo ni mtoto wa nani.

Nikiongea na mzee mmoja aliyeishi na familia ya Mwalimu kwa miaka mingi lakini akakataa kutajwa kwenye makala hii, amenieleza kwamba si kweli kwamba Mkapa anaielewa vizuri familia ya Mwalimu.

Mzee huyo anasema Mkapa anamuelewa zaidi Mwalimu kiofisi. Anasema Mkapa alikuwa akija pale Msasani akiwa mwandishi wa rais, anapewa maelekezo ya kazi na kuondoka. Eti alikuwa hashindi pale wala kulala. Kwahiyo eti haikuwa rahisi kwake kumuelewa kila mtoto aliyekuwa na uhusiano na Mwalimu ikizingatiwa pale kwa Mwalimu walikuwa wanakuja watoto wengi jamaa zake Mwalimu.

Kitu kingine ni kwamba, katika moja ya kauli zake zenye utata alizozitoa akiwa Arumeru, Mkapa aliwaambia wana Arumeru yeye alizaliwa CCM na kukulia CCM! Ni nani asiyeona kuwa kauli hiyo inadhihirisha ninachokisema hapa kwamba daima anaamini kuwa wananchi wana uvivu wa kufikiri?

Mzee Mkapa aliyezaliwa mwaka 1938 anawezaje kudai kuwa kazaliwa CCM wakati chama hicho kimeanzishwa mwaka 1977? Hata kama alikuwa ana maana ya kuanzia TANU bado alikuwa amewaweka wananchi majaribuni kwa sababu wakati chama hicho kinaanzishwa tayari yeye alikuwa kijana mkubwa tu, hakuna namna anayoweza udai alizaliwa wakati wa chama hicho.



Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company