Jukwa la wahariri Tanzania wakosowa kufungiwa Mtanzania na Mwananchi

Absalom Kibanda

Watoto wa shule ya msingi wakisoma magazeti kwenye kibanda cha kuuza Magazeti Kivukoni Front , Dar es Salaam
Jukwaa la wahariri Tanzania linasema kwamba sababu zilizotolewa na serikali kufunga kwa mufda magazeti ya Mtanzania na Mwananchi, hazina msingi wa kweli, kwa sababu hakuna ushahidi wowote wa watu kulalamika na hakuna ushahidi wa habari zozote za kuchochea habari zozote za kuchochea.

Seikali ya Tanzania iliyafungia magazeti hayo mwishoni mwa wiki kutokana na tuhuma za kuandika habari na makala za uchochezi. Akitoa tamko la serikali, Mkurugenzi wa Idara ya habari, Assah Mwambene alisema kuwa serikali imefikia uwamuzi huo kutokana na habari za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani na vyombo vya dola na kuhatarisha amani na mshikamano nchini humo.


Akizungumza na Sauti ya Amerika, Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania Absalom Kibanda anasema "uwamuzi huo bado unakumbusha namna serikali yetu inavyoendelea kutumia sheria zile zile kandamizi dhidi ya vyombo vya habari."

Kufuatana na uwamuzi wa serikali gazeti la Mtanzania limefungiwa kuchapisha kwa muda wa siku 90 kuanzia Septemba 27 na gazeti la Mwananchi limefungiwa kwa siku 14.

Bw. Kibanda ambae pia ni mhariri mtendaji wa Shirika la New Habari anasema uwamuzi huo unarudisha nyuma uhuru wa vyombo vya habari na unatokana na hofu zisizona maana za baadhi ya viongozi wa serikali kwamba vyombo vya habari vinazidi kuwa na ushawishi mkubwa kuweza kueleza ukweli wa mambo. Na hatua kama hiyo inaweza kuvitishia kutoeleza ukweli wa mambo
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company