Papa John Paul II na John XXIII wanatarajiwa kutangazwa watakatifu Aprili 27 mwakani, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa sasa wa kanisa Katoliki, Papa Francis.
Taarifa ya uamuzi huo imetolewa leo kwenye mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, ikiwa ni hatua mihimu ya kuthibitisha tangazo lake la Julai mwaka huu kwamba atawapa heshima viongozi hao wawili wa juu wa Kanisa waliopita katika karne ya 20.
www.hakileo.blogspot.comKatika taarifa iliyonakiliwa kutoka kwenye gazeti la mtandaoni la Daily Mail, alisema wakuu hao wa Kanisa Katoliki duniani ambao kwa sasa ni marehemu waliweza kutumia karama zao kwa uamunifu na kuonyesha matendo makuu.
Wachambuzi wa masuala ya Kanisa hilo alieleza kwamba inaonekana umuzi huo ni wa makusudi ikiwa ni hatua ya kujaribu kuliunganisha kanisa hilo ambalo lina mkanganyiko kwa sasa.
Kila mmoja ana watu wanaomuunga mkono na wanaompinga, ambapo kwa sasa Francis anaonekana kuungwa mkono na wote wa pande zote mbili hivyo kuwa kichocheo cha kuunganisha na kufuta makovu yaliyolikumba Kanisa hilo kwa miaka ya hivi karibuni.