Kampeni za uchaguzi zimepamba moto nchini Ujerumani zikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya siku ya siku kuwadia.
Kampeni za uchaguzi zimepamba moto nchini Ujerumani zikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya siku ya siku kuwadia.
www.hakileo.blogspot.com
Mabango ya uchaguzi yaliyotundikwa katika kila ukuta wa nyumba na milingoti ya taa majiani nchini Ujerumani yanaamstaajabisha anasema Mazen Hassan ambae ni mtaalam wa masuala ya kisiasa kutoka Misri.Si ya kutukanana hivyo kama nilivyofikiria anasema.Mwenzake Vasiliki Georgiadou wa kutoka Ugiriki amevutiwa zaidi na kauli mbiu ya bango la kampeni ya uchaguzi kutoka chama cha siasa kali za mrengo wa kushoto die Linke inayosema:"Mia bin mia kwaajili ya jamii".Hakuna kutukanana hata kidogo katika kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani.Chunrong Zehng anakenua na kusema "kila vyama vinapokuwa vikubwa ndipo nayo mabango ya kampeni yanapokuwa makubwa na ya kuvutia."
Kindani ndani lakini mabango hayo hayana chochote anasema mtaalam huyo wa masuala ya kisiasa kutoka China.Anatoa hoja akisema kwamba SPD na CDU vinatanguliza mbele sifa za wagombea wao na sio yaliyomo katika ratiba zao za uchaguzi.
Zoezi la uchaguzi
Georgiadou,Hassan na Zheng ni miongoni mwa wataalam 20 wa masuala ya siasa za Ujerumani kutoka kila pembe ya dunia walioalikwa na shirika la Ujerumani la ushirikiano katika sekta ya taaluma DAAD kusimamia kampeni za uchaguzi wa september 22 nchini Ujerumani.
Uchaguzi na hatimae muundo wa serikali ni jambo linalomvutia zaidi anasema Mazen Hassan ambae ni mtaalam wa masuala ya kisiasa katika chuo kikuu cha Cairo."Kwetu sisi ni jambo la kusisimua kuona jinsi vyama vidogo vidogo vinavyoweza kushawishi utaratibu wa kuunda serikali ya muungano-anasema .Au pia jinsi chama cha SPD ambacho ni cha pili muhimu nchini Ujerumani,kinapowekwa kando ikiwa CDU/CSU na waliberali wanaunda serikali ya muungano.Cha kusisimua zaidi anasema mtaalam huyo wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Cairo ni :"Werevu wa wajerumani katika kupiga kura na njia tofauti zinazojitokeza katika kuunda serikali ya muungano-yote haya ni yanaivutia sana Misri."
Lakini idadi kubwa ya wananchi wa Misri hawafuatilizii zoezi hili la uchaguzi anasema Hassan anaehisi wamisri wanajishughulisha zaidi na matatizo ya siasa ya ndani.
Jee AfD watawakilishwa bungeni?
Kinyume na China ambako zoezi hili la uchaguzi linafuatiliziwa kwa makini anasema Chunrong Zheng wa kutoka chuo kikuu cha Tongji cha Shanghai.Seuze tena Ujerumanai ni mshirika mkubwa wa China barani Ulaya.
Hata katika vyombo vya habari vya Ugiriki uchaguzi wa Ujerumani na hasa chama kinachopinga sarafu ya Euro,Chaguo Mbadala kwa Ujerumani AfD unafuatiliziwa kwa makini,anasema kwa upande wake Georgiadou ambae ni mtaalam wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Panteion mjini Athens.