Rais Barack Obama wa Marekani hana mipango ya kukutana na rais wa Iran Hassan Rowhani kujadili mgogoro wa taifa hilo kuhusu mpango wake wa nyuklia, pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Uvumi kuhusu kuwepo mkutano huo unamuhusu kiongozi huyo aliyeingia madarakani Agosti mwaka huu, ambae amejieleza kutaka kujihusisha zaidi na mataifa ya magharibi zaidi ya mtangulizi wake Mahmoud Ahmadinejad umetoweka.
Naibu mshauri wa masula ya usalama, Ben Rhodes amesema "kilichopo ni kujihusisha kwa uwazi kabisa na Iran lakini kwa msisitizo maneno yao yafuatane na vitendo". Aidha alibainisha kwamba kwa mara kadhaa rais Obama ameacha milango wazi ya mazungumzo na Wairan. Obama na Rowhani kwa pamoja wamepangwa kuzungumza Jumanne ijayo huko makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
www.hakileo.blogspot.com
Aidha Obama atakutana na Rais Mahmoud Abbas pembezoni mwa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza tangu kuanza upya mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.
Tatizo la wakimbizi wa Syria
Wakimbizi wa Syria wakiwa katika kambi ya Zaatari, nchini Jordan wakiwa wamekusanyika kuomba jumuiya ya kimataifa kuwasaidia
Mkutano huo wa Jumanne unafanyika kabla ya ule wa uliyopangwa na Ikulu ya Marekani, unaomuhusu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Septemba 30. Obama vilevile atakutana na Rais wa Lebanon Michel Suleiman kujadili wimbi la wakimbizi kutoka nchi jirani ya Syria.
Vilevile intarajiwa atakutana na rais wa Nigeria Goodlulc Jonathan, kuzungumzia jitihada za kukuza uchumi barani Afrika na ushirikiano wa usalama katika kukabiliana na wanamgambo wa kundi la waislamu wenye itikadi kali Boko Haram.
Rowhani kuzungumza na Hollande
Kwa kutumia mtandao wake wa twitter Ijumaa, Rowhani amesema atakutana na rais wa Ufaransa Fracois Hollande. Na rais Omar al-Bashir wa Sudan anaetafutwa na mahakama ya uhalifu ICC, kutokana na uhalifu wa kivita na mauwaji ya halaiki, amepangwa kuzungumza Ijumaa katika mkutano huo wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Wanaharakati wa haki za binadaamau wamelaani kiongozi huyo kuiwakilisha Sudan katika mkutano huo mkubwa wa kimataifa.
Kwa upande wake Marekani ilikataa kuzungumza chochote iwapo Bashir anapewa visa ya kuingia nchini humo au la. Pamoja na kuwepo kwa utata wa kisheria wa rais huyo lakini Marekani kama taifa mwenyeji wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa inapaswa kuruhusu wakuu wote wamataifa kuhudhuria mkutano huo.