MAKALA, SOMA JINSI SHERIA KUTOKA INDIA ILIVYO KOMBOA VYOMBO VYA HAZABARI

Sheria ya haki ya kupata Habari inayotumika nchini India imeleta maendeleo makubwa katika uwajibikaji wa viongozi wa umma pamoja na kuwa na uwazi na kuendeleza mbele utawala bora na demokrasia.nkazawaindia 200 200
Akizungumza na ujumbe wa wabunge na wajumbe wa Baraza la wawakilishi katika ukumbi wa Bunge la Lok Sabha iliyoko New Delhi India Katibu wa Kamisheni Kuu ya Habari ya India Tarun Kumar alisema kuwa sheria hiyo imeleta mabadiliko ya uwajibikaji pamoja na watu kuweza kufahamu haki zao ikiwemo haki ya kupata Habari.

“Hii ni sheria muhimu ambapo imeleta ufanisi na uwajibikaji wa viongozi na pia imeendeleza demokrasia ya kweli hapa nchini India tokea kuanzishwa kwake mwaka 2005”, alisisitiza.
Alisema kuwa katika kufanikisha kwa kutunga sheria hiyo taasisi na asasi mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia pamoja na Vyombo vya Habari vilishirikiana na kuwa na mshikamano na baadae serikali nayo ilishirikiriana wa vyombo hivyo na kuweza kutungwa kwa sheria hiyo.
Akifafanua zaidi alisema kuwa haki ya kupata Habari imesaidia kuwapa uwezo wa kuhoji na hususan inawahusu zaidi sehemu na Vyombo vya serikali na hivyo huwajibika kutoa habari pale wananchi wanapohoji.
Alisema kuwa katika kuimarisha utendaji wa sheria ya haki ya kupata Habari serikali imeweka watu maalum ambao kazi yao ni kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa sheria hiyo na hali iliyowezesha wengi kuweza kupata ufafanuzi katika masuala wanayohitaji.
“Kifungu cha 4 (1) c katika sheria ya Haki ya Kupata Habari ya India imetoa haki ya wananchi kupata habari na zinapatikana kwa kadri inavyotakiwa na wananchi pale wanapoona kuna haja ya kufanya hivyo”,alisema
Aidha alikiri kuwa kila sheria ina mipaka yake na hivyo sheria hii ya haki ya kupata Habari imetoa tamko la baadhi ya mambo ambayo hayatakiwi kutolewa hadharani bali yatakuwa katika mipaka ya wahusika pekee.
“Kifungu cha 8 kimeleeza bayana mambo ambayo hayatakiwi kutolewa hadharani ikiwemo masuala yanayohusu usalama wa nchi masuala ya kiuchumi na pia pale habari hiyo inaweza kuhatarisha usalama wa muhusika”, alifafanua.
Alikiri kuwa serikali ya India kwa nyakati tofauti imekuwa na mashirikiano makubwa katika kuimarisha sheria hiyo lakini pia imetoa nafasi ya watu wote hata wale wasiojua kusoma na kuandika kuweza kufaidika na sheria hiyo na huweza kupata usaidizi katika kuandika hoja za kile wanachotaka ufafanuzi.
“Serikali imejitahidi kuweka maofisa wa habari ambao kazi yao kuweza kuwasaidia kuandika katika lugha wanayoifahamu watu wa kawaida waliopo vijijini na hivyo sheria hiyo imeweza kutelekelezwa kwa ufanisi na kuwafikia zaidi ya watu bilioni moja wa India” alisisitiza.
Naye mwenyekiti wa Baraza la Habari la India Jaji Markandey Katju alisema kuwa sheria ya haki ya kupata habari ni muhimu katika kuleta ufanisi wa kazi na kuimarisha demokrasia endelevu.
Ili nchi iweze kutekeleza kwa vitendo demokrasia ya kweli kuwa na sheria ya haki ya kupata Habari ni kitu ambacho kamwe hakiwezi kuepukika.
“Sheria ya haki ya kupata Habari ni muhimu na ni ya lazima ikiwa nchi yeyote inataka kutekeleza kwa vitendo demokrasi ya kweli utawala bora uwajibikaji pamoja na kuimarisha demokrasia”, alisisitiza.
Alikiri kuwa pamoja na ubora wa sheria hiyo, baadhi ya wakati imekuwa na vipingamizi na baadhi ya watu wamekuwa wakiitumia vibaya huku wakitoa vitisho kwa viongozi na baadhi ya wakati wamekuwa hata wakidai rushwa na hongo.
Wabunge na wajumbe wa Baraza la wawakilishi wamo katika ziara ya siku tano nchini India ikiwa ni sehemu muhimu ya kuendeleza masuala ya haki ya kupata Habari Tanzania, na kujifunza jinsi gani sheria hiyo imeweza kufanikiwa nchini India.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company