GAZETIIB LA MWANCHI KUREJEA KWA KISHINDO KESHO



HABARI ZETU


Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL) Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji leo wa gazeti la Mwananchi lililokuwa limefungiwa kwa wiki mbili. Kulia kwake ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky na kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bernard Mukasa. 

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, wachapishaji na wauzaji wa magazeti ya MWANANCHI, MWANASPOTI, na THE CITIZEN leo imetoa ufafanuzi katika mambo mawili, kuhusiana na tukio lililotokea hivi karibu. Kwanza ni gazeti lake mama la MWANANCHI ambalo halikuchapishwa wala kuuzwa kwa takribani majuma mawili kwa agizo la serikali. Kuhusiana na hilo, wameongelea kuhusu KUREJEA KWA 

UCHAPISHWAJI WA GAZETI HILOna KUUSHUKURU UMMA kwa kuwa nao bega kwa bega.

KUREJEA KWA UCHAPISHAJI WA GAZETI

Kwa mujibu wa agizo la Serikali, kutochapishwa kwa gazeti la Mwananchi kunakwisha leo, na kuanzia kesho tarehe 11.10.2013 gazeti litakuwa mitaani kama kawaida. Kwa hiyo kuanzia kesho wasomaji wa gazeti hilo maarufu wataendelea kupata gazeti lenye habari za uhakika zinazojikita kwenye umahiri, uhuru, na weledi wa uandishi na uhariri.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando, magazeti hayo yataendelea kusambazwa nchi nzima na kufika mapema kabisa kote, kupitia kwa mawakala na wauzaji wake walioenea kote Tanzania.

Kwa wapenzi wa gazeti la Mwananchi waliopo jijini Dar es Salaam, kesho watauziwa magazeti na waandishi wa gazeti hilo ambao kuanzia asubuhi watakuwa mtaani wakisherehekea uhuru wao kwa kukutana na wasomaji wao moja kwa moja.

PROMOSHENI YA CHOMOKA NA MWANANCHI

Kutochapishwa kwa gazeti la MWANANCHI kwa majuma mawili kulisababisha ile promosheni ya CHOMOKA NA MWANANCHI isimame kwa muda huo huo. Tido alichukua Fursa kuwajulisha wasomaji wake kwamba promosheni hii sasa inarudi tena na inaendelea kuanzia ilipokuwa imekomea. Zawadi za shilingi milioni moja kila siku, na zawadi za magari mapya, zitaendelea kushindaniwa na kutolewa ili kutimiza ile ahadi yetu ya kutoa zawadi zenye thamani ya jumla ya shilingi 250,000,000/=

www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company