Kenya yasema itashirikiana na dunia katika mapambano dhidi ya ugaidi

Ris Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliahidi kuwa serikali yake itashirikiana na jumuiya ya kimataifa katika mapambano dhidi ya ugaidi ili kulinda utulivu wa Kenya, na Kenya haitatishwa na magaidi. Akiongea na balozi wa Marekani nchini Kenya Bw Robert Godec, Rais Kenyatta amesema Kenya itafanya kazi kwa karibu na jumuiya ya kimataifa katika mambo yote ya usalama yenye manufaa kwa Kenya, Afrika Mashariki na dunia.

Balozi Godec amesema serikali ya Marekani iko tayari kutoa msaada wowote ambao Kenya inahitaji katika mapambano dhidi ya ugaidi. Kwa sasa wataalamu wa Marekani wako katika jengo la Westgate lilishambuliwa na magaidi wa kundi la Al Shabaab, wakiendelea kuwasaidia maofisa wa Kenya kutafuta miili ya watu na ushahidi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company