
Wizara ya mshikamano wa kijamii ya Misri imeamua kulivunja kundi la Muslim Brotherhood kama shirika lisilo la kiserikali.
Wizara inayoshughulikia kutoa leseni ya kuundwa kwa mashirika hayo baadaye itakutana na waandishi wa habari ili kuzungumzia zaidi suala hilo. Hapo jana kamati ya baraza la mawaziri iliamuru kuondolewa kundi la Brotherhood katika orodha ya serikali ya mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyopewa vibali. Awali, mahakama ya Cairo iliamuru kupigwa marufuku kwa shughuli zote za kundi hilo, kuzuia fedha na kuunda jopo la kusimamia mali za kundi hilo.www.hakileo.blogspot.com
