
China itashikilia sera ya mageuzi na ufunguaji mlango bila kulegalega, na ina imani na maendeleo endelevu ya uchumi wake. Hayo yamesemwa na rais Xi Jiping wa China wakati akihutubia mkutano wa wadau wa sekta ya viwanda na biashara wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC unaofanyika huko Bali, Indonesia. Rais Xi amesema China inatarajia kuwa nchi za Asia na Pasifiki zitashirikiana ili kuijenga kanda hiyo iongoze kiuchumi duniani, kuzinufaisha pande mbalimbali na watu wa kizazi kijacho.
Katika hotuba yake iliyozungumzia "kuhimiza mageuzi na ufunguaji mlango na kujenga mustakabali mzuri wa kanda ya Asia na Pasifiki", rais Xi amesema hivi sasa, kazi ya kufufua uchumi wa dunia ni ngumu, na uchumi wa kanda ya Asia na Pasifiki pia unakabiliwa na changamoto mpya. Ama nchi zilizoendelea au zile zinazoendelea, zote zinatafuta injini mpya ya kuleta ongezeko.
Anasema, "injini ya ongezeko itatoka wapi? Naona itapatikana tu kutokana na mageuzi, marekebisho na uvumbuzi. Nchi mbalimbali za Asia na Pasifiki zinapaswa kuwa na ujasiri katika kuanzisha njia ya kuendeleza uchumi huria unaohimiza uvumbuzi na ongezeko na maslahi ya pamoja, ili kanda ya Asia na Pasikifi ioneshe uongozi katika kufufua uchumi wa dunia."
Kutoka mkutano wa kundi la nchi 20 uliofanyika St. Petersburg hadi mkutano huu wa APEC kisiwani Bali, rais Xi Jinping amekuwa akieleza imani yake juu ya mustakbali wa uchumi wa China. Imani yake inatokana kuwa uchumi wa China unaongezeka kwa asilimia 7.6, kiwango ambacho kinaridhisha na kinafikia lengo lililowekwa, pia inatokana na ongezeko tulivu lenye sifa na ufanisi wa maendeleo ya uchumi, fursa za ongezeko zinazatokana na upanuzi wa miji ya aina mpya, nguvu kazi ya kizazi kipya, mkakati wa kupata maendeleo kwa kufanya uvumbuzi, mahitaji na matumizi katika soko kubwa la China, na pamoja na mustakbali mzuri wa maendeleo ya Asia na Pasifiki.
Anasema, "uchumi wa China umeingia kwenye kipindi kipya cha maendeleo ambapo njia ya kupata maendeleo inafanyiwa mageuzi makubwa na muundo wa uchumi wa China unarekebishwa. Mchakato huo ni mgumu wenye changamoto nyingi. Lakini baada ya dhiki, faraja. China inapaswa kuimarisha mageuzi na ufunguaji mlango ili ipate maendeleo zaidi."
Rais Xi amesisitiza kuwa China itajitahidi kujenga mfumo wa ushirikiano kati ya nchi zilizopo kando ya Bahari ya Pasifiki na kunufaisha pande mbalimbali.
Anasema, Inapaswa kuonesha uongozi na uratibu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki, kuendelea kutekeleza sera ya kufungua mlango, kuridhisha pande zote na kunufaishana, kuimarisha uratibu wa sera ya uchumi wa jumla, kuhimiza uratibu wa biashara huria ya kanda, kuimarisha mchakato wa utandawazi, kuzihimiza nchi zilizopo kando ya Bahari ya Pasifiki zijenge uhusiano wa kiwenzi ili kupata maendeleo endelevu.www.hakileo.blogspot.com
