HATIMAE Wabunge nchini Marekani wakubaliana kuidhinisha fungu la fedha kunusuru Serikali


Rais wa Marekani, Barack Obama
REUTERS/Yuri Gripas
Na Emmanuel Richard Makundi

Wabunge wa bunge la Congress na lile la wawakilishi wamepitisha muswada wa sheria utakaoruhusu kupatikana kwa fedha zinazofikia kiasi cha trilioni 16, fedha ambazo sasa zinawezesha kufunguliwa kwa shughuli za serikali hadi mwezi January mwaka 2014.

Hapo jana wabunge wa Congress walipitisha kwa kishindo mapendekezo ya chama cha Democrats na yale ya Republican na mapema leo asubuhi bunge la Seneti na lenyewe likapigia kura muswada huo ambao wabunge 256 waliunga mkono mkono.

Muswada huo sasa unatarajiwa kuwasilishwa kwa rais Barack Obama ambaye amesema atautia saini mara moja ili kuona shughuli za serikali zikianza haraka baada ya kuwa zimesimama kwa muda kutokana na kukosekana kwa fedha.

Kupitishwa kwa muswada huo kunatoa nafasi ya kufunguliwa kwa ofisi za serikali na kujiendesha hadi tarehe 15 january mwaka 2014 jambo ambalo hatahivyo linaonekana kuwa bado halijatatua tatizo.

Katika hatua nyingine rais Barack Obama amewapongeza wabunge wa Republicans na wale wa chama chake kwa kufikia makubaliano ili kuruhusu Serikali kujiendesha.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company