Kugunduliwa kwa maiti za watoto wadogo wanne zilizopatikana katika vitongoji vya kandokando ya jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini kumewashtua watu wengi nchini humo.
Jumanne iliyopita polisi ya Afrika Kusini iligundua maiti za watoto wadogo wawili wa kike waliokuwa na umri wa miaka miwili na mitatu katika eneo la watu maskini la Diepsloot lililoko umbali wa kilomita 45 kaskazini mwa Johanneburg. Suala hilo lilizusha machafuko na vurugu za wakazi wa eneo hilo waliotaka kujua sababu za mauaji hayo na kuilaumu serikali kwamba imeshindwa kulinda usalama wa raia wake.
Siku moja baadaye yaani Jumatano ya jana polisi ya Afrika Kusini iligundua maiti nyingine mbili za watoto wadogo wa kike waliokuwa na umri wa mwaka mmoja na miaka mitatu katika eneo la Katlehong; suala ambalo limezusha wasiwasi mkubwa nchini Afrika Kusini kuhusu usalama wa watoto wadogo.
Polisi inafanya uchunguza kubaini iwapo watoto hao walinajisiwa kabla ya kuuawa au la.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amelaani vikali mauaji hayo akisema kuwa ni mateso makubwa ambayo hayawiani na jamii inayojengwa na Waafrika Kusini
www.hakileo.blogspot.com