Tanzania yalalamika kutengwa na mataifa mengine ya EAC

wakulima wa Afrika Mashariki wahudhuria warsha juu ya namna ya kuimarisha mazao yao.
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania imezungumzia hatua ya baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC za Kenya, Uganda na Rwanda kufanya mikutano kati ya nchi tatu kujadili masuala ya jumuiya hiyo pasipo kuzishirikisha nchi za Tanzania na Burundi.

Tanzania kupitia wizara hiyo ya ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema kuwa pamoja na kuwa mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC unaruhusu nchi wanachama kuwa na ubia, ni lazima suala linaloenda kutekelezwa chini ya mfumo huo liwe limejadiliwa na kukubalika na nchi zote wanachama.

Katika mikutano kati ya nchi tatu, Kenya, Uganda na Rwanda, uliofanyika june 24 hadi 25 Entebbe Uganda, wajumbe walikubaliana juu ya mambo mbali mbali ua miundo mbinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mombasa kuelekea Kigali kupitia Kampala, ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Sudan Kusini kupitia Uganda hadi Kenya na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta Uganda.

Zauidi ya hayo walijadili juu ya kuongeza namna ya kupata umeme zaidi, kuanzisha mfumo moja wa forodha, kuharakisha Shirikisho la Kisiasa, vitambulisho vya kitaifa kutumika kama hati ya kusafiria na visa ya pamoja ya utalii.

Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Vedastina Justinian amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumatatu kwamba kufuatia hali hiyo, baraza la mawaziri la Afrika Mashariki limemtaka Mwenyekiti wa baraza la mawaziri ambae ni waziri wa mambo ya Kigeni wa Uganda kutoa taarifa ya kina kuhusu mikutano iliyofanywa na athari zake kwenye utangamano wa Jumuiya ya Afrika Masharki katika mkutano wa 28 wa baraza la mawqaziri unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu mjini Arusha.

Hata hivyo Tanzania imesema ikiwa ni sehemu ya mtangamano huo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ina nia ya kuhakikisha inatekeleza makubaliano ya pamoja kulingana na matakwa ya Mkataba wa kuanzishwa jumuiya hiyo unaotaka kushirikisha pia wananchi katika kila hatua.

Tanzania katika mkutano wa 27 wa baraza la mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Arusha Agosti 31 mwaka huu ilitaka kujua hatma ya mtangamano wa jumuiya ya afrika mashariki na kutaka ufafanuzi kutokana na ukweli kwamba baadhi ya mambo ambayo nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zinayajadili na kuyatolea amaamuzi , bado majadiliano yake yanaendelea katika ngazi ya jumuiya.

Mkutanano mwingine wa baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo ya afrika mashariki ambako ndiko kutatolewa ufafanyzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi ujaoa
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company