UTAFITI MWINGINE WAIMBUA TENA SERIKALI,WAONESHA TZ INAONGOZA AFRIKA KWA WANANCHI WAKE KUWA NA WASIWASI.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya kupunguza umaskini (REPOA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrobarometer kwenye nchi 35 barani Afrika, umeonyesha kwamba nchi ya Tanzania inaongoza kwa Wananchi wake kuwa na wasiwasi juu ya matukio ya uhalifu ikilinganishwa na nchi nyingine yoyote ile ya Afrika.

Mkurugenzi mtendaji wa REPOA Samuel Wangwe anakwambia kiwango cha wasiwasi kimeongezeka mpaka asilimia 40 ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2003/2008 lakini pia vilevile kwenye rekodi ya uhalifu, Tanzania kwenye utafiti huu haiko juu sana wala chini sana yani katikati ila kwa Wananchi kuhisi kama kuna uhalifu utatokea ndio Tanzania imeshika number one.


Afisa mwandamizi mipango wa jeshi la Polisi Beatus Silla amesema ‘Ulinzi shirikishi utapunguza hili tatizo ambalo utafiti umesema, vituo vya polisi viko mbali na wale wanaohitaji huduma, tumepeleka askari 258 pamoja na pikipiki hawa Askari watakaa na Maafisa wa idara mbalimbali katika kutatua matatizo mbalimbali katika maeneo yao’
www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company