Israel yawatumia Waafrika kama panya wa maabara

 NA IRIB KISWAHILI
Imebainika kuwa Israel, Marekani pamoja na shirika la madawa la Pfizer huwatumia wanawake Waafrika kama panya wa maabara kufanyia majaribio dawa ya kupanga uzazi ambayo inaweza kufunga kabisa kizazi na kuua. Ripoti zinasema kuwa majaribio hayo ya kinyama ya madawa ni thibitisho jingine la utambulisho wa kibaguzi wa utawala haramu wa Israel ambao umekuwa ukiwabagua wahamiaji Mayahudi kutoka bara la Afrika. Kwa mujibu mtaalamu wa Marekani Dakta Randy Short aliyehojiwa na Press TV, wanawake Mayahudi Waafrika wanaoishi Israel wanapewa dawa za kupanga uzazi ambazo zimeshapigwa marufuku katika nchi nyingi kutokana athari zake mbaya ikiwa ni pamoja na kusababisha kifo kwa anayezitumia. Aidha kumefichuliwa ushirikiano wa serikali ya Marekani na shirika la madawa la Pfizer katika kuhimiza utumizi wa dawa hizo hatari za kupanga uzazi. Weledi wa mambo wanasema hiyo ni njama ya kupunguza idadi ya wanawake wa Kiafrika wenye uwezo wa kuzaa. Dawa hiyo ya kupanga uzazi ijulikanayo kama Depo-Provera imetajwa kuwa hatari sana na inaenezwa kote Afrika katika fremu ya kampeni inayogharimu zaidi ya dola bilioni moja na inayoongozwa na Bill Gates. Dakta Randy Short anasema Depo-Provera ambayo imepigwa marufuku Canada na Ulaya husababisha saratani, ukimwi, kudhoofika mifupa n.k. Mtaalamu huyo ameongeza kuwa wahajiri wa Kiafrika huko Israel si tu kuwa wanatumika kama panya wa maabara bali pia viungo vyao muhimu vya mwili kama figo huondolewa na kuuzwa bila idhini yao.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company