Wanajeshi wa Uganda waingia Juba, Sudan Kusini

 NA REDIO IRAKHAN
Duru za habari kutoka Uganda zinasema kuwa, wanajeshi wa Uganda wako Juba, makao makuu ya Sudan Kusini kwa shabaha ya kudhamini usalama na amani katika mji mkuu wa nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa na Uganda baada ya kuombwa rasmi na serikali ya Sudan Kusini. Taarifa zinasema kuwa, kikosi maalumu cha Uganda kimechukua jukumu la kudhamini usalama katika uwanja wa ndege wa Juba na kuwaondoa raia wa Uganda waliokuwa mjini humo. Luteni Kanali Paddy Ankunda Msemaji wa Jeshi la Uganda amesema kuwa, umetumwa ujumbe nchini Sudan Kusini kwa lengo la kuratibu njia za kuwaondoa raia wa Uganda katika mji wa Juba. Luteni Kanali Ankunda amesema kuwa, kundi la kwanza la raia wa Uganda tayari limeshawasili nchini Uganda. Inafaa kuashiria hapa kuwa, jumla ya watu 500 wameuawa baada kujiri mapigano katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba pale wanajeshi wanaoaminika kuwa watiifu kwa Riek Machar makamu wa zamani wa Rais, walipojaribu kuipindua serikali ya Rais Salva Kiir.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company