Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIAF) Ijumaa ya leo limeanza mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la Ghuba ya Uajemi kusini mwa nchi.
Luteka hiyo inajumuisha vikosi kutoka vituo vyote vya IRIAF na ni sehemu ya awamu kuu ya mazoezi makubwa yaliyopewa jina la Fada'eeyan-e Harim-e Velayat 4 (Walinzi wa Anga Takatifu za Wilayat 4).
Msemaji wa luteka hiyo Hussein Chitforoushan amesema mazoezi hayo ya siku mbili yatajumuisha ndege za kivita, ndege za kijeshi za kubeba mizigo, ndege za upelelezi wa kijeshi, ndege za kulinda doria baharini na ndege zisizo na robani. Ameongeza kuwa idadi kubwa ya ndege za kivita zinazotumika katika mazoezi hayo zimetengenezwa hapa nchini Iran. Mazoezi hayo pia yanajumuisha oparesheni za masafa marefu ambapo ndege za kivita zitaongezwa mafuta zikiwa zinapaa angani. Aidha makombora kadhaa yatafanyiwa majaribio katika luteka hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni Iran imekuwa ikifanya mazoezi ya kijeshi baharini, angani na nchi kavu. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwa kwa mara imesisitiza kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi ni wa kujihami.