Baadhi ya wapiganaji waasi wa kiislamu ambao wanamahusiano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda
Na
RFISyria imetangaza Saudi Arabia kuwa ni adui yake wa kwanza kwa tuhuma za Saudi kujaribu kuitibua Syria kwa kufadhili silaha kwa makundi ya wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali na waasi wanaopigana kumuondoa madarakani raisi wa Syria Bashar Al Assad.
Taifa hilo la kiarabu lenye utajiri wa mafuta limekuwa likisaidia upande wa upinzani tangu kuanza kwa machafuko ya nchini Syria mnamo mwezi March 2011 huku serikali ya Saudi ikitoa wito wa kuangushwa kwa utawala wa Assad.
Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa syria Faisal Muqdad ameiambia AFP kuwa Saudi Arabia imeendelea kuyasaidia makundi ya kigaidi nchini Syria wakati huu ambao mataifa mengine yamekuwa yakipitia upya nafasi zao kuhusu mzozo wa Syria.