Waislamu wanaounga mkono kundi la Seleka nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati waandamana kwa kupinga kile wanachosema majeshi ya Ufaransa yanaegemea upande wa Wakristo


Wanajeshi wa wa kikosi cha Umoja wa Afrika kutoka Burundi wakipiga doria mjini BanguiREUTERS/Alain Amontchi

Na RFI

Maelfu ya waislamu jijini Bangui katika Jamahuri ya Afrika ya Kati waliandamana jana Jumapili kupinga Operesheini ya majeshi ya Ufaransa kuwapokonya silaha waasi wa Seleka nchini humo.

Katika Oparesheni hiyo wanajeshi wa Ufaransa wamewauawa waasi waatu wa Seleka akiwemo kiongozi mmoja, mauji ambayo yamewakasirisha waislmau nchini humo ambao wanadai kuwa majeshi ya Ufaransa yamekuja nchini humo kuwalinda Wakiristo
Madai ya wandamnaji hayo yamekanushawa vikali na majeshi ya Umoja wa Afrika MISCA yanayolinda amani nchini humo .

Msemaji wa majeshi ya umoja wa Afrika nchini Afrika ya Kati, Eloi Yao, amesema, majeshi ya Umoja wa Afrika hayaegemeyi upande wowote, na lengo lao ni kuhakikisha makundi yote yanayomiliki silaha yanapokonywa.

Maandamano hayo yaliendelea jana mchana hadi katika mtaa unaoishi waislamu wengi ambao unajulikana kwa jina la PK5.

Waandamanaji walikua na vibango vinavyoandikwa,”Hollande muuwaji”, “Hatuitaki Ufaransa !”.

Awali waandamaji waliweka viziwizi kwenye barabara kuu inayounganisha manispa ya jiji la Bangui na uwanja wa ndege, lakini baadae askari polisi wa majeshi ya Umoja wa Afrika (Misca) kutoka jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo waliwatawanya.

Wakati huohuo, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inajiandaa kuwatuma askari wengine wapatao 850 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kulinda amani, hasa kwa vile nchi hiyo ina ujirani wa urefu wa kilomita 1, 570 na DRC na tayari imewapokea wakimbizi elfu 50 tango mgogoro huo uanze.

Takribani wanajeshi 1600 wa Ufaransa walitumwa nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati katika operesheni ya kuyapokonya silaha makundi yanaozimiliki kinyume cha sheria, operesheni inayo julikana kwa jina la Sangaris.

Zaidi ya nusu ya wanajeshi hao wanapiga kambi mjini Bangui.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company