'Watoto wanauawa kikatili Jamhuri ya Afrika ya Kati'


Takriban watoto wawili wanaripotiwa kuuawa kwa kukatwa vichwa tangu kuanza kwa ghasia huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mapema mwezi uliopita wa Desemba.
Mjumbe wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Souleymane Diabate anasema kuwa dhulma zinazofanyika dhidi ya watoto ni za kutisha ikiwemo kuingizwa jeshini na pia wanalengwa wakati wa kulipiza kisasi.

UNICEF na washirika wake wamethibitisha kuuawa kwa karibu watoto 16 na kujeruhiwa kwa karibu ya wengine 60 tangu ghasia zianze kushuhudiwa mjini Bangui tarehe tano mwezi uliopita wa Desemba

Machafuko ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yamepelekea zaidi ya watu milioni moja kuwa wakimbizi ndani ya nchi hiyo. Katika siku za hivi karibuni mji wa Bangui umekuwa ukishuhudia maandamano ya wananchi wanaotaka kuondoka vikosi vamizi vya Ufaransa nchini humo. Waandamanaji wanasema kuwa, askari wa Ufaransa waliotumwa nchini humo kwa madai ya kurejesha amani na utulivu, wamezusha hitilafu zaidi na mgawanyiko mkubwa kati ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company