Kamisheni ya haki za binadamu ya Afrika imekosoa hukumu ya kunyongwa iliyotolewa kwa mamia ya wanachama wa harakati ya Ikwanul Muslimin ya Misri. Kamisheni ya haki za binadamu ya Afrika imeitaka serikali ya mpito ya Misri kutotekeleza hukumu hiyo ya kunyongwa dhidi ya wanachama wa Ikhwanul Muslimin na badala yake ianzishe uchunguzi kuhusu kutolewa hukumu hiyo ya mahakama. Taasisi hiyo ya haki za binadamu pia imemtumia barua Rais Adly Mansour wa Misri na kuafiki kufuatiliwa suala hilo. Serikali ya mpito ya Misri inawajibika kutekeleza maamuzi ya kamisheni ya haki za binadamu ya Afrika kwa sababu Cairo imesaini hati ya Kiafrika kuhusu haki za binadamu.