Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amepinga pendekezo lililotolewa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) la kuitaja harakati ya Ikhwanul Muslimin kuwa ni kundi la kigaidi. Akiwa safarini hivi karibuni huko Saudia, Ramtane Lamamra Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria alisema kuwa Algiers inapinga pendekezo hilo la wakuu wa Riyadh la kutaka kuitambua harakati ya Ikhwani kuwa ni kuwa ni kundi la kigaidi. Algeria imesema kuwa haiwezi kuchukua hatua nje ya mantiki ya sheria na bila ya kuwa na ushahidi kwa kuyatuhumu makundi ya Kiislamu ikiwemo harakati ya Ikhwanul Muslimin.
Ripoti za vyombo vya habari vya Algeria zinaeleza kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo amewasilisha ushauri mbalimbali kwa Saudi Arabia na Imarati kuhusu uzoefu mchungu uliopitia Algeria katika kipindi cha muongo mmoja wa ugaidi wa umwagaji damu uliopelekea makumi ya maelfu ya raia kuwa wahanga na kuhusu namna ya kuamiliana na mirengo mbalimbali ya Kiislamu nchini humo. Wakati huo huo baadhi ya duru zimeeleza kuwa, Algeria imeitaka Saudi Arabia itoe orodha ya shakhsia wanaotuhumiwa katika kesi za ugaidi na ushahidi unaothibitisha tuhuma dhidi ya shakhsia hao na kwa njia hiyo watuhumiwa hao waweze kujumuishwa katika faharasa ya magaidi.