Mwana Mfalme wa Saudi Arabia ameeleza mshikamano wake na kwamba yuko pamoja na mabinti wa Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia wambao wamewekwa chini ya kifungo cha nyumbani katika mji wa Jeddah nchini humo. Katika ujumbe alioutuma katika ukurasa wake wa Facebook, mwana mfalme Khalid bin farhan al Saud amewasifu binti mfalme Sahar na dada zake watatu kwa kuunga mkono mapambano ya raia waliodhulumiwa wa mji wa Qatif katika mkoa wa kaskazini wa huko Saudi Arabia.
Mwana mfalme Farhan alijitenga na familia hiyo ya kifalme mwezi Julai mwaka jana akisema kuwa utawala wa Saudi Arabia haujasimama kwa misingi ya sheria za Mwenyezi Mungu. Mwana mfalme Khalid bin Farhan al Saud ametoa matamhsi hayo baada ya binti wa mfalme aliye na umri wa miaka 42 kuwataka wananchi wa Saudia kuendeleza maaandamano yao dhidi ya utawala wa Aal Saud. Sahar, Maha, Hala na Jawaher al Saud ni mabinti wa Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia ambao inasemekana kuwa hivi sasa wako katika kifungo cha nyumbani huko Jeddah.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago