CHANZO http://kiswahili.irib.ir/
Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amemtaka Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ayachane makubaliano yaliyotiwa saini hivi karibuni kati ya Harakati ya Muqawama ya Palestina Hamas na chama cha Fat-h ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina. Netanyahu ameongeza kuwa, utawala wa Israel hautafanya mazungumzo ya amani na serikali ya Palestina itakayoiunga mkono harakati ya Hamas. Utawala wa Israel siku ya Alhamisi iliyopita ulitangaza rasmi kusimamishwa mazungumzo ya amani kati ya utawala huo na Mamlaka ya Ndani ya Palestina, baada ya makundi ya Kipalestina ya Fat-h na Hamas kutiliana saini makubaliano ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa. Licha ya utawala ghasibu wa Israel kukosoa vikali makubaliano hayo ya Wapalestina, nayo serikali ya Washington kupitia Jennifer (Jen) Psaki Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani imesikitishwa na makubalano hayo na kusisitiza kwamba serikali yoyote itakayokuja madarakani huko Palestina inapaswa kufungamana na suala la 'kutokuwepo muqawama' na 'uwepo wa taifa la Israel'.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago