CHANZO http://kiswahili.irib.ir/
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa amani inawategemea wataalamu wa hapahapa nchini na kwamba hakuna uwezekano wowote wa kuwapokonya elimu waliyo nayo wataalamu hao wa Kiirani. Dakta Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo baada ya kukutana na Philippe Marini Mkuu wa Kamati ya Fedha ya Baraza la Seneti la Ufaransa mjini Tehran na kusisitiza kwamba uhusiano wa Tehran na Paris umerejea katika nafasi yake halisi. Zarif amesema kuwa, serikali ya Ufaransa ina nafasi muhimu katika Umoja wa Ulaya, hivyo inaweza kuitumia fursa hiyo muhimu katika mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea kati ya Iran na kundi la 5+1. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kwamba, miradi ya nyuklia ya Iran inafanyika kwa malengo ya amani, na kubainisha kwamba Iran imeingia kwenye mazungumzo hayo kwa irada ya kisiasa. Zarif amesema kuwa, Tehran ina matumaini kwamba kundi la 5+1 nalo litaonyesha nia njema kwenye mazungumzo hayo. Naye Mkuu wa Kamati ya Fedha ya Bunge la Seneti la Ufaransa ameeleza kuridhishwa na makubaliano ya awali yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili mwezi Novemba mwaka jana na kusisitiza kwamba mahusiano ya Paris na Tehran yatazidi kuimarishwa katika nyanja zote.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago