TANZANIA YAITOA KENYA U20 KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA

TIMU ya soka ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeitoa Kenya katika Raundi ya Kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Senegal kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya bila kufungana nyumbani na ugenini.
Kwa matokeo hayo, Ngorongoro inayofundishwa na kocha mzalendo John Simkoko sasa itamenyana na Nigeria katika hatua inayofuata.

Kikosi cha Ngorongoro kilichoitoa Kenya leo

Penalti za Tanzania zilikwamishwa nyavuni na Mohammed Hussein, Kevin Friday, Mange Chagula na Iddi Suleiman, wakati Mudathir Yahya alikosa.
Penalti za Kenya zilifungwa na Geoffrey Shiveka, Timonah Wanyonyi na Victor Ndinya, wakati Evans Makari na Harison Nzivo walipoteza.
Hakuna kipa aliyeokoa penalti bali wapigaji waliokosa walipiga nje.
Ilikuwa mechi kali na ya ushindani na makipa wa timu zote mbili, Aishi Manula wa Tanzania na Farouk Shikhalo wa Kenya aliyeanza kabla ya kumpisha Boniface Barasa dakika ya 88 walifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo ya hatari.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company