HATIMAE KAMPUNI YA PROIN PROMOTIONS LIMITED YASAINI MKATABA NA MZEE YUSUPH KWAAJILI YA KUSAMBAZA FILAMU YAKE IITWAYO NITADUMU NAE

Mzee Yusuph (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa filamu yake ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo imeingia sokoni leo Jumatatu na inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampun ya Proin Promotions Limited, Evans Stephen.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kwa Makini Mzee Yusuph wakati akiongelea Ujio wa Filamu yake Mpya iitwayo NITADUMU NAE ambayo imeingia sokoni leo na filamu hiyo inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited

Mzee Yusuph (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Meneja Wake Said Mwangushi (kulia) na Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Evans Stephen (Kushoto) mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa Habari leo katika ofisi za Kampuni ya Proin Promotions Limited zilizopo Mtaa wa Ursino Mikocheni

Mzee Yusuph akibadilishana Mkataba na Mwanasheria wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Halima Mara baada ya Kumaliza kutiliana saini katika Mikataba.

Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited
Hatimaye Mzee Yusuph atambulisha rasmi ujio wake katika Tasnia ya Filamu leo mara baada ya kuitambulisha filamu yake mpya na ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo ni moja ya filamu ambazo zimetoka katika nyimbo zake.


Akiongea na Waandishi wa Habari Mzee Yusuph alisema "Filamu hii nimeitengeneza muda mrefu sana na imetoka katika nyimbo zangu lakini nilishindwa kuisambaza kutokana na kukosa Msambazaji ambaye anaweza kukubaliana na vigezo vyangu lakini Kwa bahati nzuri Proin Promotions imeweza kuwa na vigezo ambavyo mimi nimekubaliana navyo na nimeridhika navyo ndio maana nimeona wanaweza kusambaza filamu yangu"


Na Pia ameelezea sababu kubwa ya yeye kuamua kufanya kazi na Proin Promotions ni kwamba "Kampuni ya Proin Promotions hainunui hakimiliki za wasanii ndio maana nimeona nifanye nao kazi"


Vilevile Filamu ya Mzee Yusuph ishaingia sokoni leo na inasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Limited ambapo filamu hiyo inapatikana Nchi nzima kuanzia leo.


Mbali na hiyo pia Mzee Yusuph amesema kuwa sasa anabadili nyimbo zake kwenda kwenye filamu kwasababu nyimbo zake zote zina uwezo mkubwa wakuwa filamu ndio maana kwa kuanza ameanza na Nyimbo yake ya Nitadumu Nae.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company