MFUNGAJI bora wa kihistoria wa Ujerumani, Miroslav Klose, ametangaza kustaafu soka ya kimataifa.
Kiasi kama cha mwezi mmoja tangu ashjinde Kombe la Dunia na nchi yake nchini Brazil, mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 ameamua kupumzika timu ya taifa.
Amefikisha jumla ya mabao 16 aliyofunga katika Kombe la Dunia na jumla ameifungia mabao 71 timu yake ya taifa. Huyo ndiye pia mfungaji wa mabao mengi zaidi katika Fainali za Kombe la Dunia, akifuatiwa na Mbrazil Ronaldo Lima mwenye mabao 15.
Mchezo umekwisha: Miroslav Klose ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya kuifungia Ujerumani mabao 71
REKODI YA MABAO YA KLOSE KOMBE LA DUNIA
1, 2, 3: Ujerumani 8-0 Saudi Arabia, makundi, 2002
4: Ujerumani 1-1 Jamhuri ya Ireland, makundi, 2002
5: Cameroon 0-2 Ujerumani, makundi, 2002
6, 7: Ujerumani 4-2 Costa Rica, makundi, 2006
8, 9: Ecuador 0-3 Ujerumani, makundi, 2006
10: Ujerumani 1-1 Argentina (baada ya dakika 120, penalti 4-2), Robo Fainali, 2002
11: Ujerumani 4-0 Australia, makundi, 2010
12: Ujerumani 4-1 England, 16 Bora, 2010
13, 14: Argentina 0-4 Ujerumani, Robo Fainali, 2010
15: Ujerumani 2-2 Ghana, makundi, 2014
16: Brazil 1-7 Ujerumani, Nusu Fainali, 2014
Klose alifunga mabao mawili Ujerumani ikitwaa Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago