Ishara hiyo yakuweka mikono juu ingali[endeza kama ingalisadifu yaliyopo |
Napata shaka kama kweli viongozi wa Afrika na jumuia zake ikiwemo EAC na AU kama wanatambua kwa umakini athari za madudu ayoyafanya Raisi huyu wa Burundi anaejianda kumwaga damu zisizo na hatia ikiwa ni wakati mchache tuu mara baada ya nchi hiyo kutoka kwenye mapigano yaliyosababishwa na vita vya weyewe wenyewe.
Lakini hili ni matokeo ya mfumo wa kijinga uliopo miongoni mwaviongozi wakuwalinda viongozi waliopo madarakani hatakama wanafanya mambo ya kijinga yanayohatarisha maisha ya watu.
Yamkini bado huja nielewa ni kwamba,katika taifa hili la Burundi mwaka huu linatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu ambao unahusisha ngazi ya Raisi,lakini kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo ni kwamba Raisi haruhusiwi kugombea kwa zaidi ya miula miwili ambayo kila muhula unahusisha mika 5,na kiongozi huyu alianza kutawala toka mwaka 2005 ambapo kwa sasa ni muhula wake wa mwisho.
Sio katiba ya nchi hiyo tuu bali hata mkataba uliomwingiza madarakani ujulikanao kama mkataba wa AMANI WA ARUSHA,ulitamka jambo hili.
Anajiandaa kukiuka kwa kutumia janja ya nyanyi eti wakati anachaguliwa mwaka 2005 kwa kuwa alichaguliwa na wabunge na sio wanchi kwa hiyo kwake ahesabu kama ni muula wa kwanza yaani anautambua tuu muhula wa pili.
Ukijuuliza sana upuuzi huu unaweza hata ukashindwa kuelewa kama huyu mtu alikuwa akitawala taifa gani wakati huo,na waliomchagua walimchagua kwa niaba ya nani?
N pia kwanini asinali kataa kutawala kwa kuchaguliwa na watu ambo kwa mujibu wa kauli yake hawakuwa na uhalali?.
Naongea haya wakati viongozi wa vyama vya upinzani na mashirika ama viongozi wa kidini wakiwa wameshaanza kulaani upuuzi huu na wengine kutishia kufanya maandamano huku yeye mwenyewe akiwatatharisha kwa kusema ole wao watakao andamana na kuwaita ya kwamba wanahatarisha usalama wa umma.
Yangu ni machache ila msije kusema OSCAR alisemaga kipindi fulani,chukuweni hatua kabla ya hayajatokea mabaya kwani nidhairi kwamba hatua na maamuzi hayo hayatavumilika kwenye hilo taifa na matoke yake ndo hayo yaliyowahi kujitokea hapo zamani.