Ndugu zangu,
Kuna matukio makubwa yalitokea sambamba na Vita Vya Kagera vilivyokuwa vikiendelea mwaka 1978. Kwenye kitabu chake ' Sowing The Mustard Seed', Yoweri Museveni anasimulia tukio la kijasusi mlengwa akiwa ni yeye.
Museveni alikuwa Nairobi kukutana na baadhi ya Waganda wanaharakati. Ndani ya intelijensia ya Tanzania, kulikuwa na mkakati wa kushawishi uasi wa kijeshi ndani ya jeshi la Idi Amin. Museveni alishirikishwa.
Pale Nairobi, Museveni alikuwa akitembea akigawa kwa Waganda wanaharakati nyaraka zenye hotuba ya Julius Nyerere.
Makachero wa Kenya walizinasa harakati za Yoweri. Wakapanga kumnasa Museveni. Walimtuma jasusi Mzungu mwenye uraia wa Kenya. Aliitwa Patrick Shaw. Huyu alikuwa jasusi lilokubuhu na inasemwa alikuwepo kwenye mpango uliotekelezwa wa kumteka na kumwua mwanasiasa wa Kenya wa enzi hizo, J. M Kariuki, mwaka 1976.(P.T)
Museveni anasimulia, kuwa alipokaa na rafiki yake akinywa kahawa mgahawani, Nairobi Hilton Hotel, ghafla, alimwona mzungu mnene mwenye madevu akiingia. Alikuwa jasusi Patrick Shaw.
Jasusi Shaw alikaa mbali kidogo na Museveni. Akachukua gazeti na kujifanya analisoma huku akitupa jicho kwa kuvizia kwa Yoweri Museveni.
Jasusi Shaw alikaa mbali kidogo na Museveni. Akachukua gazeti na kujifanya analisoma huku akitupa jicho kwa kuvizia kwa Yoweri Museveni.
Museveni akafanya maamuzi ya haraka, akamwambia rafiki yake abaki hapo hapo. Naye Museveni akakunjua gazeti kujifanya yuko bize analisoma. Kisha akaagiza kahawa nyingine. Muhudumu alipokuja nayo tu, basi, Museveni, akainuka kujifanya anakwenda haja ndogo. Ikawa kimoja...breki ya kwanza ikawa Namanga.
Nini kilimtokea Museveni alipofika Namanga, bila passsport wala nyaraka nyingine za kumwezesha kuvuka mpaka kuingia Tanzania?
Kesho nitasimulia, panapo majaliwa...
Maggid,
Iringa.
Iringa.