Moto uliozuka mapema leo katika nyumba moja iliyopo kati ya mtaa wa Jamhuri na Mosque jijini Dar es Salaam na kuteketeza mali kadhaa ambazo bado haijaulikana thamani yake. Mashuhuda waliokuwepo wakati moto huo ukianza kuwaka wanafikiri moto huo huenda umesababishwa na hitilafu ya umeme lakini msemaji kutoka kikosi cha zima moto amesema chanzo kamili cha moto huo bado hakijajulikana.
Wasamaria wakiliondosha gari lililokua karibu na jengo hilo.
Kikosi cha zimamoto na Jeshi la Polisi wakiwa eneo la tukio. Picha zote kwa hisani ya Michuzi Blog. (P.T)
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago