CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Geita kimesema kimebaini kwa kituo hewa cha kujiandikisha wananchi kwenye daftari la wapiga kura kiitwacho Buharahara “B” katika kata mpya Bomba Mbili.
Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Geita, Nguru Tanganyika, alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema Chadema haikitambui kituo hicho ambacho kipo kinyume na makubaliano yaliyokuwapo kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Magareth Nakainga na vyama vyote vya siasa.
Tanganyika alisema wamekibaini kituo hicho hewa kutokana na jitihada za viongozi wa chama hicho kutembelea vituo mbalimbali vya kujiandikishia.
“Ofisi ya Chadema wilaya ya Geita kama mdau wa uchaguzi, imebaini kituo hewa cha Kata ya Bomba mbili kinyume na makubaliano kati ya Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi wa Mji wa Geita na vyama vya siasa.
“Tulikubaliana hakutakuwa na uandikishaji wa wapiga kura Kata ya Bomba mbili kwa kuwa haijakidhi vigezo vya sheria kufanya uchaguzi kwa sababu ya kukosa wakazi wanaotosheleza kupiga kura.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago