KUANZISHA HUDUMA YA HOSPITALI INAYOTEMBEA

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) iliyopo jijini Dares Salaam inatarajia kuanzisha huduma ya hospitali inayotembea kwa kutumia gari maalum mara baada ya kukakamilisha mchakato wa gharama za matibabu kupitia mfumo huo.

Hayo yalisemwa leo Dkt. Gimmy Temba kutoka Kitengo cha Dharura cha MNH na kwenye maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijijni Dares Salaam.

“ Tuna magari mawili ya hospitali inayotembea ambayo tunapata msaada kutoka nchi ya Japan yenye vifaa kisasa kwa ajili uchunguzi wa matibabu ya dharura wa mgonjwa ,” alisema.

Alisema hivi sasa wako katika mpango wa kuangalia namba maalum ambazo zitakuwa zinatumika wakati mgonjwa anapokuwa akihitaji huduma hiyo. Hivyo namba hizo zitakapo kuwa tayari watazitangaza kwa wananchi ili waweze kuzifahamu.

Aliongeza kuwamba magari ya hayo yako mawili nchi nzima na yatakuwa yanatoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa dharura, pia wanatarajia kupata magari mengine mawili .

Alivitaja baadhi ya vifaa vilivyoko katika magari hayo kuwa ni mashine ya kuangalia mzunguko wa damu na hewa, kusukuma damu,kupumzisha ikiwemo ya kuondoa uchafu mfano vile damu au mate.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company