JK KUHUSU MRITHI WAKE KWENYE URAIS

Kuna jambo ambalo limepewa kipaumbele sana Magazetini toka wameanza kujitokeza Wagombea Urais wa CCM, swali jingine ni kwamba eti Rais JK ana mtu ambae anamuandaa kumrithi?

Majibu yako kwenye hizi sentensi 10 nilizomnukuu ”Mchakato wa Uchaguzi umeanza kwenye Vyama vya Siasa... Na sisi tumeanza mchakato kwenye nafasi ya Urais, watu wamejitokeza kwa wingi na ni nzuri kwa Demokrasia“ Rais Kikwete.

“Mmoja alinitumia message akasema umenisaidia sana kufika hapa naweza kushika hata hiyo nafasi yako, nipe baraka zako.. nikamwambia ‘goodluck‘ sasa sijui ataitumia hiyo goodluck yangu kusema mzee amenichagua mie!”

“Mimi sina mtu wa chaguo langu, Chama kitatusaidia kupata Kiongozi mzuri na makini... Kama wanaogombea kwenye Vyama wataamua kupigana vikumbo mpaka kutumia na misuli itakuwa imezidi, itabidi Serikali kuingilia kati... lakini kwenye majukwaa watu kusema sisi ndio zaidi ya wale hiyo haina maneno wala haileti ugomvi“Rais Jakaya Kikwete.

Hapa utamsikia Rais JK mwenyewe akijibu ishu hiyo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company