MISWADA 7 MIPYA YA SHERIA YATUA BUNGENI

SERIKALI imewasilisha bungeni miswada sita mipya ambayo imesomwa jana kwa mara ya kwanza.

Aidha, miswada saba inatarajia kujadiliwa na kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote katika vikao vitakavyoanza Juni 29 hadi Julai 8 mwaka huu.

Miswada iliyosomwa kwa mara ya kwanza jana ni ule Muswada wa Sheria ya Benki ya Posta Tanzania kwa mwaka 2015 iliyolenga kufuta sheria iliyosajili benki hiyo ili sasa isajiliwe chini ya Sheria ya Makampuni.

Mwingine ni Muswada wa Sheria ya Vituo vya Pamoja Mipakani wa 2015, Muswada wa Sheria Uwazi na Uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania wa mwaka 2015.

Pia umo Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato na Mafuta ya Gesi wa mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Petroli wa mwaka 2015.

Kwa mujibu ratiba iliyotolewa kwenye mtandano wa Bunge, miswada itakayojadiliwa na kupitishwa ndani ya siku 10 kuanzia Juni 29 ni wa Sheria ya Kupata Habari wa mwaka 2015, Muswada ya Sheria ya Tume ya Walimu, Muswada wa Sheria ya Kufuta Benki ya Posta, Muswada wa Sheria ya Kituo cha Pamoja Mipakani.

Mingine ni Muswada wa Sheria ya Petroli na Gesi, Muswada wa Sheria Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uchimbaji Tanzania na Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato na Mafuta ya Gesi na Muswada wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015. (HABARI LEO)
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company