|
Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis (kushoto) na Alexis Tsipras (kulia) vinatarajiwa kukutana leo Jumatatu na wafadhili wa Ugiriki kujaribu kufikia makubaliano katika zikisalia siku chache ili kufikia tarehe ya mwisho. REUTERS/Alkis Konstantinidis |
Na RFI
Ugiriki na wafadhili wake wanakutana leo Jumatatu ili kutafuta mkataba wa daharura, baada ya waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro mwishoni mwa wiki hii.
Marais na viongozi wa serikali wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro wanakutana Jumatatu wiki hii katika mkutano wa dharura jijini Brussels nchini Ubelgiji, baada ya kutoafikianakatika mkutano uliyofanyika juma lililopita mjini Luxembourg. Lengo : kuepuka Ugiriki kushindwa kulipa madeni yake.
Kwa upande wa wafadhili, hisia ya kutoaminiana imetawala, kabla ya mkutano wa kidiplomasia unaolenga kuboresha mazungumzo na kuleta imani kwa wafadhili juu ya Ugiriki. Mkutano ambao unatazamiwa kufanyika Jumatatu wiki.
Hakuna mtu hata mmoja katika mkutano huu, ambaye anataka kutoa maoni juu ya mapendekezo mapya yaliyotangazwa siku ya Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita na Alexis Tsipras. Mapendekezo ambayo yangeweza kufikia " mkataba ambao si wa muda, lakini wa kudumui ", amesema waziri mkuu wa Ugiriki, ambaye anatarajia kufutwa kwa sehemu ya madeni ya Ugiriki na hatua kali kuchukuliwa.
Mapendekezo ambayo mwenyekiti wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker, ameyataja kwenye akaunti yake ya Twitter "msingi mzuri kwa ajili ya maendeleo", bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi juu ya yaliyomo katika mapendekezo hayo.
Benki kuu ya Ulaya inapaswa kuamua kama inaongeza kwa mara nyingine tena, kiwango cha fedha ambacho inaweza kukopa mabenki ya Ugiriki, ikiwa ni utaratibu wa dharura ambao utapelekea kudhibiti mfumo wa benki za Ugiriki ambazo ziko njiani kufilisika. Kwa sababu hatima ya Ugiriki haitegemei nia njema ya Angela Merkel, Christine Lagarde na Jean-Claude Juncker, lakini inategemea ile ya Mario Draghi, mkuu wa zamani wa benki ya kimataifa ya Marekani kimataifa Goldman Sachs.