Askari polisi mjini Bujumbura akijielekeza katika eneo la shambulio la gruneti, Julai 21, 2015.
AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Na RFI
Hali ya usalama imeendelea kudorora katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura. Tangu Jumatatu mwanzoni mwa juma hili milio mingi ya risasi na milipuko ya magruneti vimeendelea kusikia katika maeneo mbalimbali ya mji huo hadi usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano.
Usiku wa Jumatatu kuamkia jUmanne kituo cha vijana wilayani Kamenge, Kaskazini mashariki mwa mji wa Bujumbura kilishambuliwa na kundi la watu waliojihami kwa silaha wasiojulikana.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Pierre Nkurikiye, haya ni mashambulizi yaliyoendeshwa kwa makusudi dhidi ya kituo cha vijana wilayani Kamenge na si dhidi ya ngome ya polis iilio karibu na kituo hicho. Pierre Nkurikiye amesema askari polisi mmoja na raia mmoja walipata majeraha madogo, lakini zaidi ya magruneti 10 na roketi moja vilirushwa katika kituo hicho. Mswmaji wa polisi amebaini kwamba kasha 200 za risasi ziliokotwa sehemu hiyo.
Katika kituo cha vijana cha Kamenge kuna kituo cha redio ya vijana inayorusha matangazo yake hapo, lakini pia kunapatikana katika kituo hicho makazi ya watawa na makazi ya makuhani, ikiwa ni pamoja na askofu Jean-Louis Nahimana, mwenyekiti waTume ya Ukweli na Maridhiano.
Askofu huyo Ameeleza kwamba hawezi kusema iwaporisasi hizo ziliyorushwa dhidi ya kituo cha vijana zilikua risasi hewa, baada ya urishianaji risasi kati ya polisi na kundi la watu wenye silaha au ilikua shambulio dhidi kituo cha redio ya jamii aidha ni mashambulizi yalikua yanawalenga wahubiri ambao wanaishi sehemu hiyo. Hata hivyo, askofu Jean-Louis Nahimana amethibitisha kuwa risasi hizo zilifikia makazi ya yao, na kusababisha uharibifu mkubwa, huku akibaini kwamba baadhi ya kuta ziliharibiwa kwa risasi.
Vyanzo vya karibu na wapiganaji vimekanusha kwamba makuhani walikuwa wamelengwa. Vyanzo hivyo vimebaini kwamba mashambulizi matano yameendeshwa usiku dhidi ya ngome za polisi, na kusema kuwa zaidi ya askari polisi 20 wameuawa.
Milio ya risasi na milipuko ya magruneti vimeendelea kusikika usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano katika wilaya za waandamanaji mjini Bujumbura, ikiwa ni pamoja na Cibitoke, Mutakura na Ngagara. Mashahidi wanasema polisi ndio imeendesha operesheni hiyo kwa minajili ya kujilipiza kisasi baada ya mashambulizi ya Jumatatu usiku.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago