Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema kuwa baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni, yeye amepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein.
Aidha, akiongea na wanahabari, Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye fomu zinazotoka vituoni.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago