Goodluck Jonathan rais wa zamani wa Nigeria kushoto
RFI Kiswahili
Na Victor Melkizedeck Abuso
Waangalizi wa Kimataifa wanasema uchaguzi Mkuu nchini Tanzania ulikuwa huru na haki, na wananchi wa taifa hilo walikuwa katika mazingira mazuri ya kupiga kura Jumapili iliyopita.
Waangalizi hao kutoka Umoja wa Afrika, muungano wa nchi za Kusini mwa Afrika SADC na wale kutoka nchi za Jumuiya ya Madola wametoa ripoti yao ya awali jijini Dar es salaam siku ya Jumanne na kusifia uvumilivu na ustaarabu wa Watanzania kipindi chote cha uchaguzi.
Umoja wa Afrika ukiongozwa na rais wa zamani wa Msumbuji Armando Emilio Guebuza, umesema uchaguzi nchini Tanzania ulifanyika kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, zile za Ukanda na zile za Kimataifa na kutii misingi ya demokrasia.
Hata hivyo, rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan ambaye anaongoza waangalizi wa nchi za Jumuiya ya Madola amesema waangalizi wa jumuiya hiyo wamekiri kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa njia ya amani na utulivu, lakini wanasubiri kumalizika rasmi kwa matangazo ya matokeo ya uchaguzi wa urais kabla ya kutoa ripoti yao ya mwisho.
“Tunaweza kusema tumeridhika kidogo na namna uchaguzi huu ulivyofanyika lakini hatuwezi kutoa ripoti kamili hadi pale tutakaposhuhudia umalizikaji wa ujumuishwaji wa matokeo ya urais,” alisema Jonathan.
Nao muungano wa wabunge kutoka nchi za Kusini mwa Afrika SADC, umetaka katiba kubadilishwa katika siku zijazo ili kuruhusu mgombea kwenda Mahakamani kupinga matokeo hasa ya urais na pia kuteuliwa kwa Makamishena wa tume ya uchaguzi kuwashirikisha wadau mbalimbali likiwemo bunge.
Ripoti ya mwisho ya waangalizi hawa inatarajiwa kutolewa baada ya mshindi wa ushindani wa urais kufahamika, huku wale wa Jumuiya ya Madola wakisema watatoa ripoti yao kamili baada ya wiki nne au sita ijayo.
Kwa sasa Watanzania wanaendelea kupokea matokeo kutoka kwa tume ya uchaguzi huku ushindani ukiwa kati ya mgombea wa chama tawala CCM John Pombe Magufuli na mgombea wa upinzani Edward Lowasa.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago