Uingereza imetoa angalizo kwamba huenda mlipuko ndio uliosababisha ndege ya shirika la ndege la Urusi kuangukia nchini Misri na kuua abiria wote mia mbili na ishirini na wanne waliokuwa kwenye ndege hiyo.
Safari za ndege kati ya nchi za Misri na Uingereza na pwani ya mapumziko ya rasi ya Sharm el-Sheikh zimesitishwa kama tahadhari wakati maofisa kutoka nchini Uingereza wakiendelea kuangalia hali ya usalama katika uwanja wa ndege.
Halikadhalika safari za kutoka na kuingia katika rasi hiyo zimesitishwa na Ireland.
Mamlaka ya safari za anga nchini Urusi hivi karibuni walitoa tahadhari kuwa ni mapema mno kuhisi nini chanzo cha ajali hiyo.
Mabaki ya ndege hiyo na kisanduku cheusi chenye kurekodi mwenendo wa ndege hiyo bado vinafanyiwa uchunguzi.
Mpaka sasa kundi la wanamgambo wa kiislamu, la Islamic State limereudia kukiri kuwa linahusika na ajali hiyo.
CHANZO BBC SWAHILI