HABARI KUU ZA LEO na OSCAR SAMBA
print this page
HABARI NA Oscar Samba
Showing posts with label makala. Show all posts
Showing posts with label makala. Show all posts

Hii ndiyo Historia ya John Magufuli wa CCM

Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza daktari John Magufuli kuwa mgombea wake

Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza daktari John Magufuli kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa ujao.

Daktari John Magufuli, alisajili asilimia 87 % ya kura za wajumbe, hiyo ikiwa ni kura 2104.

Daktari John Magufuli, aliwashinda wapinzani wake Bi Amina Salulm Ali na dakta Asha-Rose Migir.

Magufuli ni Nani?

Lakini je Daktari John Magufuli ni Nani? Daktari John Magufuli ni Nani?

Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.

Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.

Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.

Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.

Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .

Alizaliwa Oktoba 1959Alianza siasa mwaka 1995

Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.

Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.

Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.

Alianza siasa mwaka 1995

Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.

Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti

Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.

Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.

Anatambulika kuwa Mchapa kazi

Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.

Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.

Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.
0 Toa maoni yako.

Mjuwe, Historia ya Samia Suluhu Hassan

Historia ya Samia Suluhu Hassan wa CCM

Ushindi wa John Pombe Magufuli wa CCM umetoa fursa kwa Bi Samia Suluhu Hassani kuhudumia taifa hilo la Afrika Mashariki kama mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa rais wa Tanzania.

Lakini Bi Samia ni nani?

Tangu kongamano la Chama tawala nchini Tanzania CCM kumteua Daktari John Pombe Magufuli Joseph kuwa mshika bendera wa CCM, Chama hicho kiliweka historia kwa kumteua Bi Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza.

Tangu Dodoma, Bi Samia aliwekwa kwenye ramani ya wanasiasa wanawake waliobobea barani Afrika.

Lakini Bi Samia Suluhu Hassanni Nani ?

Bi Samia Suluhu ana umri wa miaka 54.

Kwa wale wanaomjua Bi Samia wanasema kuwa ni mchache wa maneno.

Asili yake ni Kisiwani Zanzibar.

Bi Samia Suluhu Hassan amewahi kushikilia nyadhifa za uwaziri katika serikali ya Muungano wa Tanzania na kadhalika amewahi kutumikia serikali ya visiwani Zanzibar kama waziri katika afisi ya makamu wa rais.

Ni mwanamke wa Kwanza kuwa Mgombea MwenzaImage captionBi Samia atakuwa naibu wa John Pombe Magufuli rais wa Jamhuri ya Tanzania

Tangazo la kumtaja kama mgombea mwenza wa rais mteule wa tano wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania sasa limezaa matunda na kumuweka Bi Samia katika mstari wa mbele barani Afrika kama naibu rais wa Jamhuri ya Tanzania.

Chama CCM pia kimeingia katika daftari la vyama vilivyowapa wanawake sauti katika serikali yake katika karne hii ya 21.

Bi Samia alikamilisha masomo ya shule ya upili mwaka wa 1976 .

Masomo

Aliajiriwa kama mchapishaji katika wizara ya mipango na maendeleo ya nchi, kazi ambayo aliifanya huku akiendelea na masomo yake hadi alipohitimu katika chuo kikuu cha Manchester, Uingereza.

Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa.

''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija.''

Kimsingi ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na uweledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya.''

''Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.

Familia

Aliolewa mwaka wa 1978, kwa Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo .

Walijaliwa watoto wanne.
Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la ZanzibarBi Samia Suluhu Hassan na rais Mteule John Magufuli

Siasa
Alijiunga na siasa mwaka wa 2000.

Wakati huo alijiunga na bunge la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.

Haikuchukua muda nyota yake ikaanza kung'aa na akateuliwa kuwa waziri na rais Amani Karume.

Alitumikia taifa hadi mwaka wa 2005 alipochaguliwa tena na kuteuliwa upya kama waziri.

Mwaka wa 2010 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi.

Punde tu akateuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano.
0 Toa maoni yako.

Fahamu sababu za Dr. Magufuli Kushinda Urais Wa Tanzania

Tanzania imeandika historia mpya, ambapo jana imempata Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli, ambaye alikuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu uliohitimishwa Jumapili ya Oktoba 25, mwaka huu.

Dk Magufuli ambaye katika kampeni ya kuwania urais alikuwa na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu, si mgeni katika safu za uongozi wa Tanzania kwa kuwa amekuwa serikalini kwa miaka 20, akishika majukumu mbalimbali ambayo yalitumiwa na Watanzania kumpima.


Moja ya sifa yake kubwa tangu alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia chama hicho mwishoni mwa Mei mwaka huu, ni uadilifu katika utendaji kazi wake katika majukumu tofauti aliyokabidhiwa Rais huyo mteule wa Awamu ya Tano, anatajwa kuwa katika majukumu yote ya kitaifa aliyowahi kukabidhiwa, alionesha sifa ya juu ya uaminifu na uadilifu, ambao umeelezwa kwa namna mbili tofauti.


Ujenzi barabara
Kwanza ni uongozi wake wa miradi mikubwa ya fedha nyingi, ambayo kwa muda wote wa uongozi wake hakuwahi kukumbwa na kashfa. Kwa mfano mwaka huu tu, alikuwa akiongoza Wizara ya Ujenzi, iliyokuwa na bajeti ya Sh trilioni 1.2 na Mfuko wa Barabara uliokabidhiwa zaidi ya Sh bilioni 866.


Katika miaka 15 aliyoongoza Wizara hiyo ya Ujenzi, katika ngazi hiyo alisimamia miradi ya zaidi ya Sh trilioni 9.5, lakini hakula hata senti tano, badala yake alijenga mtandao mrefu wa barabara za lami nchi nzima.

Usimamizi
Namna ya pili ya kuzungumzia uadilifu wake ni usimamizi wake wa watendaji na wadau wa sekta ya ujenzi, ambao amekuwa akiwapa kazi za mabilioni ya shilingi na kuisimamia kwa karibu katika kuwatumikia Watanzania.


Dk Magufuli amekuwa akisimamia makandarasi zaidi ya 8,500, wahandisi zaidi ya 15,000 na wakadiriaji majengo zaidi ya 1,300, ambao wamekuwa wakinufaika na kazi za Serikali za mabilioni ya shilingi.


Kama angetumia vibaya nafasi hiyo na angetaka kumuomba au kushinikiza kila mmoja wao ampe Sh milioni moja tu kwa mwaka, angeweza kujikusanyia pato binafsi lisilo halali la zaidi ya Sh bilioni 100 kila mwaka. Pamoja na kuwa karibu na kishawishi hicho, lakini Dk Magufuli hakushiriki kuhujumu hata senti moja na hana historia wala hakuwahi kutajwa popote kutumia vibaya nafasi yake hiyo katika sekta yenye maslahi makubwa ya kifedha.


Ukali kwa wazembe
Badala ya kuomba michango ya kujinufaisha kutoka kwa wadau hao wa ujenzi, Dk Magufuli alijikuta akifukuza kazi makandarasi zaidi ya 3,000 wa ndani na nje ya nchi, bila kujali utajiri wao, pale makandarasi hao walipozembea kazi au kufanya kazi chini ya kiwango.


Namna ya tatu inayotumika kuelezea uadilifu wa Dk Magufuli, imeelezwa mara kadhaa na Jaji Joseph Warioba, ambapo alisema mwaka 1996 alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuongoza Tume ya Kero za Rushwa, alikuta sekta ya ujenzi ikinuka rushwa kubwa. Lakini, anafafanua kuwa baada ya Dk Magufuli kuanza kufanya kazi katika sekta hiyo, kelele ya rushwa katika sekta hiyo imetoweka. Uchapakazi Mbali na uadilifu, Dk Magufuli pia anatajwa kuwa mchapakazi.


Hata Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi mara kadhaa amempa jina la ‘simba wa kazi’, huku Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake, akimpa jina la ‘tingatinga’ ambalo huwa halishindwi kazi katika mazingira yoyote ya ujenzi, huku wananchi wengine wakimuita ‘jembe’. Matokeo ya uchapakazi wake, yanaonekana katika sekta ya ujenzi, alikofanya kazi kwa miaka 15 tu, ambapo amefanikiwa kusimamia ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya kilometa 17,700.


Kazi hiyo imeweka historia ambayo hata wakoloni, Wajerumani na Waingereza, waliotawala Tanganyika wakati huo tangu mwaka 1884/1885 mpaka wakati wa Uhuru mwaka 1961, zaidi ya miaka 75 walijenga mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa 1,360 tu.

Wasifu wake
Dk Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 Chato (sasa Mkoa wa Geita), hivyo jana alipotangazwa kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, ambapo alitimiza miaka 56.


Dk Magufuli ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 1991 – 1994 alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza. Mwaka 1985 – 1988 alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1981 – 1982 alisoma Diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.


Kati ya mwaka 1979 – 1981 alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Juu ya Sekondari Mkwawa, Iringa. Mwaka 1977 – 1978 alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza. Mwaka 1975 – 1977 alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera. Mwaka 1967 – 1974 alisoma Shule ya Msingi, Chato. Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mpwapwa mkoani Dodoma.


Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha. Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.

Uzoefu wa kazi
Kuanzia mwaka 2010 alikuwa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato. Mwaka 2008 – 2010 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato). Mwaka 2005 – 2008 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).


Mwaka 2000 – 2005 Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka 1995 – 2000 Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka 1989 – 1995 Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Co-operative Union (Ltd) Mwanza. Mwaka 1982 – 1983 Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati). Amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.


Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa. Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.

Mchakato wa urais
Dk Magufuli alitangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa Mei mwaka huu, baada ya CCM kutangaza rasmi ratiba ya mchakato wa urais kwa wanachama wake. Aliingia kwenye harakati za kuwania nafasi ya urais kimya kimya, tofauti na makada wengine wa CCM ambao walihutubia Taifa.


Lakini, kimya chake kiliufanya mchuano wa uchaguzi wa nafasi hiyo ndani ya CCM, uliokuwa na wagombea 42 kuwa mkali zaidi. Baada ya hapo, waliorejesha fomu walikuwa wagombea 38 na kati ya hao baada ya kujadiliwa na vikao vya juu vya Chama, ikiwemo Kamati Kuu, wagombea watano - Dk Magufuli, Bernard Membe, Dk Asha Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ally na January Makamba, ndio waliofanikiwa kupelekwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.


Baada ya Nec, ambako wagombea hao walijadiliwa na kupigiwa kura, Dk Magufuli, Balozi Amina na Dk Migiro ndio waliofanikiwa kuingia tatu bora, ambapo walifikishwa katika Mkutano Mkuu na kuomba kura na baada ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano huo, akapatikana Dk Magufuli kupeperusha bendera ya CCM.

Ahadi zake Dk
Magufuli katika mikutano yake ya kampeni, alikuwa akiahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi aliosema atapigania kila mmoja awe na kazi ya kumpa kipato, wajenge nyumba bora.


Katika kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, Serikali yake itatoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake na vijana. Mbali na kutoa mikopo hiyo izunguke katika ngazi ya kijiji na mtaa, Dk Magufuli pia alisema Serikali yake itazuia kila aina ya usumbufu, unaofanywa kwa wafanyabiashara hao, ikiwemo kukamatwa kwa bodaboda na mama ntilie.


Kwa wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao kwa kuwa atahakikisha mbali na wakulima kupata bei nzuri ya mazao yao, watakapoiuzia Serikali itakuwa bidhaa kwa fedha taslimu.

Aidha, aliahidi kuondoa ushuru unaosumbua wafanyabiashara wadogo na wakulima, ili wafanye biashara kwa uhuru wajipatie kipato halali.


Dk Magufuli pia alisema baada ya kusambaza umeme, atahakikisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vinajengwa vijijini ili kusindika mazao ya kilimo shambani ili kutoka shambani bidhaa za mazao hayo ziuzwe katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kuhusu migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, Dk Magufuli aliahidi kukabiliana na migogoro hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa ardhi zaidi kwaajili ya wakulima na wafugaji, ili kuondoa uhaba wa ardhi uliosababisha ugomvi wa maeneo ya kulishia mifugo na kulima.


Lakini pia aliahidi kunyang’anya mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila kutumiwa, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya kilimo.

Katika elimu, alikuwa akiahidi kuhakikisha kuanzia mwakani, wanafunzi kutoka darasa la awali mpaka kidato cha nne, wanasoma bila kulipa ada, ili kuondolea wazazi usumbufu wa watoto wao kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada.


Kwa wanafunzi wa elimu ya juu, aliwahakikishia kuwa hakutakuwa na usumbufu wa kupata mikopo na kuwataka wanahusika na kazi hiyo, kuwa tayari kwa kuwa atataka kila mwenye sifa ya kusoma elimu ya juu, apate mkopo.

Katika sekta ya afya, aliahidi kujenga zahanati kwa kila kijiji na mtaa, kituo cha afya kwa kila kata na hospitali ya rufaa katika kila mkoa, na ameahidi kukomesha kero ya kukosekana dawa katika hospitali za Serikali.


Katika kero ya maji, alikuwa akisema kama amefanikiwa kujenga zaidi ya kilometa 17,700 za barabara ya lami, hatashindwa kujenga mabwawa na mtandao wa mabomba kwenda kwa wananchi ili kukomesha kero hiyo.


Pia aliahidi kujenga barabara mbalimbali za lami za kuunganisha wilaya na za mijini, huku akiahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi, ifanane na ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), taasisi aliyoianzisha na kuitetea, ambayo leo watu wengi wanatamani kuitumikia kutokana na maslahi mazuri na mafanikio yake.
0 Toa maoni yako.

Haya hapa, MAJIMBO 10 YA KUFA AU KUPONA

Wagombea ubunge wa majimbo 10 wana kazi ya ziada ya kufanya kabla ya Jumapili wakati wananchi watakapopiga kura kuamua ushindani mkali uliotanda kwa karibu miezi miwili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu, kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi.

Ushindani huo mkubwa unatokana na vyama vya wagombea hao kuwekeza nguvu nyingi kwenye majimbo ili kuyarejesha, kuyalinda au kuwaengua wagombea ambao wanaonekana kuwa watakuwa wasumbufu iwapo watafanikiwa kuingia Bunge la 11. 

Mkoani Iringa, majimbo ya Iringa Mjini na Kilolo yana ushindani mkali.Jimbo la Kilolo linawaniwa na wagombea kutoka vyama vinne, Venance Mwamoto wa CCM, Taji Mtuga (ACT Wazalendo), Brian Kikoti (Chadema) na Lameck Mgimwa wa Chausta.

Hata hivyo, upinzani mkali unaonekana kuwa kwa Mwamoto, ambaye amerejea tena kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kuenguliwa kwenye kura za maoni za CCM mwaka 2010, na Kikoti, ambaye nguvu yake inatokana na kuungwa mkono na vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Ushindani huo unaelezwa kuanzishwa na mpasuko ndani ya CCM ulitokana na kura za maoni. Baada ya Mwamoto kumshinda Profesa Peter Msolla, aliyekuwa mbunge, na baadhi ya makada wa chama hicho kutimikia Chadema.

Mkazi wa Kilolo, Paulo Ngayomela, aliyekuwa mpambe wa Msolla, alisema yeye na wenzake walimuaga mbunge huyo wa zamani na kuungana na kambi ya upinzani baada ya kutoridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea ndani ya CCM.

Mwamoto, ambaye aliangushwa na Profesa Msolla mwaka 2010, alisema bado ana nafasi ya kushinda kwa kuwa ni kama anatetea jimbo kwa kuwa aliliongoza jimbo hilo kuanzia mwaka 2005 hadi 2010.

Iringa Mjini

Jimbo jingine gumu kutabiri ni Iringa Mjini ambalo linawaniwa na Robert Kisinini wa DP, Daudi Masasi (ADC), Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema, Chiku Abwao (ACT Wazalendo) na Frederick Mwakalebelea wa CCM.

Hata hivyo, Mchungaji Msigwa anayetetea kiti chake na Mwakalebela ndiyo wanaonekana kupambana vikali.

Mwakalebela anabebwa na falsafa inayotumiwa na CCM za kukomboa jimbo ambayo imefanikisha kuvunjwa makundi yaliyoundwa na wagombea wa nafasi hiyo wakati wa kura za maoni.

Mmoja wa makada wa chama hicho, Abdallah Mpogole alisema kwa sasa wanachama wote wameshikamana na wanachoangalia ni ushindi.

Hata hivyo, kada mmoja wa Chadema, Mussa Ali alisema: “Tukubali tusikubali tangu jimbo lilipoanzishwa, hakuna aliyefanya kazi kama Msigwa akiwa mbunge. Alipigania masilahi ya wakazi wa Iringa ikiwamo ujenzi wa barabara, maji na kutoa misaada ya vitanda katika Hospitali ya Wilaya ya Iringa.(P.T)


Jimbo hilo linaangaliwa kwa karibu na uongozi wa kitaifa wa vyama hivyo. Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa alikuwa wa kwanza kupita Iringa Mjini na kuvuta maelfu ya watu. Lakini Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli alifuta nyayo zake alipopita muda mfupi baadaye.

Ilemela

Mkoani Mwanza, Jimbo la Ilemela lina mchuano kutokana na CCM kutaka kulirejesha kutoka Chadema waliolitwaa mwaka 2010. CCM imemsimamisha Anjelina Mabula kupambana na mbunge anayemaliza muda wake, Highness Kiwia wa Chadema.

Kada wa CCM na mkazi wa Kata ya Kirumba, Yusuf Juma alisema uchaguzi wa Jimbo la Ilemela hauna mvutano kama Nyamagana, kwa sababu mgombea amekuwa na ushawishi mkubwa kuliko mwenzake wa Chadema.

Hata hivyo, mkazi wa National ambaye ni mfuasi wa Chadema, Shadrack Magafu alipinga akisema uchaguzi mwaka huu umekuwa mgumu kutokana na kila mtu kuhubiri mabadiliko.

Bukoba Mjini

Hali pia ni ngumu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera, ambako ushindani ni mkali zaidi ya ule wa mwaka 2005. Linawakutanisha wagombea ambao ni mahasimu wakubwa, Wilfred Lwakatare wa Chadema, na Balozi Khamis Kagasheki wa CCM.

Wakati Kagasheki akitetea jimbo hilo kwa kipindi cha tatu, mshindani wake anawatumia makada wa CCM waliohamia upinzani kujiimarisha kisiasa akiwamo aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk Anatory Amani aliyehamia NCCR- Mageuzi iliyo ndani ya Ukawa.

Kundi la Dk Amani lililojiunga linaongezewa nguvu na aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM wa Manispaa ya Bukoba, Chifu Karumuna aliyehamia Chadema na kuongeza ushindani, huku Balozi Kagasheki akitajwa kuungwa mkono na wanawake wengi.

Baadhi ya wakazi wa Bukoba wanafananisha ushindani uliopo sasa na ule wa mwaka 2005. Mkazi wa Mtaa wa Miembeni, Levina Paul alisema anaona ushindani mkubwa.

“Wanawake wengi tunamuunga mkono Kagasheki tofauti na inavyoonekana kwa vijana, ila wagombea wote wanaweza kuwa na nguvu sawa,” alisema Paul.

Musoma Mjini

Mkoani Mara, vita kali inaonekana Jimbo la Musoma Mjini, kati ya Vincent Nyerere wa Chadema na Vedastus Mathayo wa CCM aliyeangushwa na mshindani wake huyo mwaka 2010.

Jimbo hilo lina wagombea tisa ambao ni Tongora Eliud (ACT–Wazalendo), Ibrahim Seleman (Tadea), Maimuna Matola (ADC), Ruttaga Sospeter (AFP), Vedastus Mathayo (CCM), Vincent Nyerere (Chadema), Gabriel Ocharo (CUF), Nyakitita Chrisant (DP) na Makongoro Jumanne (UMD).

Mkazi wa mjini hapa, Leonard Lugwisha alisema kati ya wagombea hao mwenye nguvu zaidi na uhakika wa ushindi ni Nyerere, kwa kuwa ndiye mbunge anayependwa na vijana na watu wengi wamechoka kuongozwa na CCM.

Moshi Mjini

Hali ni mbaya zaidi Moshi Mjini, ambako wagombea wa CCM na Chadema wanachuana vikali kumrithi Philemon Ndesamburo ambaye ameamua kutogombea.

CCM imemsimamisha Davis Mosha na Jaffar Michael anagombea kwa tiketi ya Chadema, ambao wamefanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa na ushindani ambao haujawahi kuonekana tangu mwaka 1995.

Mkazi wa Soweto, George Mberesero alisema ushindani wa vyama hivyo viwili ni mkubwa na kueleza kuwa kama si makosa ya kiufundi, CCM ingepata kura kuliko miaka ya nyuma.

“Huko nyuma ni kama CCM ilikuwa inafanya utani kwenye kampeni lakini safari hii imefanya kampeni,” alisema Mberesero.

Mfanyabiashara Patrick Boisafi alisema awali CCM ilianza vizuri harakati za kukomboa jimbo, lakini vurugu zimewatia doa.

Mkazi mwingine wa jimbo hilo, Goodluck Moshi alisema: “CCM wanaenda nyumba kwa nyumba, lakini Chadema wanaenda mitaani. Vijana wengi wa mtaani si wa jimbo hili. Davis anakubalika kwenye kata zenye watu wengi kama Njoro na Bomambuzi,” alisema.

Katika jimbo hilo, wagombea wa vyama vya ACT-Maendeleo, Buni Ramole na Issack Kireti wa SAU hawana nguvu.

Kawe

Jijini Dar es Salaam, nguvu ya Ukawa na CCM imeelekezwa Jimbo la Kawe ambako CCM imemsimamisha Kippi Warioba na wakati Chadema imeendelea kumuamini mbunge aliyemaliza muda wake, Halima Mdee.

Inaelezwa kuwa Kippi anategemea ushawishi wa baba yake, Jaji Joseph Warioba, ambaye apia ameshasimama jukwaani kumpigia debe mwanaye.

“Watu wanaweza kumchagua kwa kumfananisha na uzalendo wa baba yake,” alisema Maria Mashasi, mkazi wa Kawe.

Hata hivyo, Aliko Mwansisya ambaye pia ni mkazi wa Kawe, alisema Mdee anayo nafasi kubwa zaidi ya kutetea jimbo hilo kutokana na ushawishi wake ndani ya Bunge.

Ubungo

Hali kadhalika, Jimbo la Ubungo lina upinzani mkali kati ya mgombewa wa Chadema, Saed Kubenea, ambaye ni mwandishi wa habari, na wa CCM, Dk Didas Masaburi, ambaye ni meya wa jiji anayemaliza muda wake.

“Kubenea ana nafasi ya kushinda kutokana na umaarufu wake na nguvu ya chama,” alisema mkazi wa Ubungo, Charles Temba.

Lakini Vicent Julius alisema pamoja na umaarufu, Kubenea atakuwa na wakati mgumu wa kushinda jimbo hilo kutokana na ushawishi, uzoefu wa Dk Massaburi.

Ushindani mkali pia upo Same Mashariki, Mtama, Vunjo, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Bunda Mjini na Ukerewe.

Imeandikwa na Geofrey Nyang’oro, Midraji Ibrahim na Phinias Bashaya na Kelvin Matandiko

Chanzo:Mwananchi
0 Toa maoni yako.

WAKENYA NA MAENDELEO,WATANZANIA NA UMASIKINI NA CCM


NIMEITOA FACEBOOK.
Achana na CCM,,,, na serekl Yake,,, inayoendelea kuyafanya,,,,, nimeikuta hii sehem,,,, naamni itazid kukupa point fulan,,,, kweny akil ya mtu anaetaka mabadiliko,,, tofaati ya wakenya na Watanzania Wakenya wanacheza smart games na Watanzania bado tumelala.. After Precision Airlines (PA) kuwa threat kwa operation za Kenya Airways (KQ) route za Tanzania na Kenya, KQ wakaingia ubia na PA very smartly na wakawa wanaihujumu undercover. Leo hii PA iko hoi na tayari Operations za Jomo Kenyatta- KIA, Jomo Kenyatta-Mwl. Nyerere zimerudi kwa KQ... Pili, baada ya TBL kuruhusiwa kuuza bia Kenya, na Kenya walete bia zao Tanzania. TBL wakakaribia kuuwa bia za Wakenya huko kwao wakati huo bia yao TUSKER ikawa haifanyi vizuri hapa Tanzania. Wakavunja makubaliano, ili kila mtu afanye biashara yake kwake. After years EABL ya Kenya ikaingia ubia na SBL na wakaipa License ya kuzalisha na kusambaza TUSKER hapa nchini.. Smartly EABL wanauza hapa kwetu wakati sisi TBL haiuzi kule kwao.. Wakati hayo yote yanafanyika Watanzania tunalazwa na fikra za kijinga za viongozi wetu wa CCM.. Education Matters alot 2004 Tanzania tulikuwa na Ndege mbili za serikali (Air Tanzania) na Kenya walikuwa na Ndege 19 (Kenya Airways-KQ).. 2015 Tanzania tuna Ndege 1 ya kukodi kwa ajili ya kupigia Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kenya wana Ndege 47 zinazotua katika viwanja 62 vya mabara yote duniani... Tukumbuke bila kuwa na Shirika letu la Ndege Utalii tunaongelea ni kazi bure.. Kenya taratibu inautawala Uchumi wa Tanzania, tayari wana Bank mbili zinazofanya kazi nchini (KCB and Equity Bank), Tanzania bado hatuna Bank yeyote Kenya. Supermarkets za Kenya tayari zimeingia nchini na kuuwa zetu (Nakumat tayari imeshainunua Shoprite (T), UCHUMI Supermarkets).. Sisi Imalaseko Supermarkets zilishakufa kule Kenya. Soko la Hisa Dar Es Salaam (DSE) lina Jumla ya Kampuni 21, kati ya hizo Kampuni 7 ni za Kikenya lakini Soko la Hisa la Nairobi (NSE) lina zaidi ya Kampuni 64 na hakuna kampuni hata moja ya Kitanzania.. Hii ni mbaya sana kiuchumi.. Serengeti National Parks ni mbuga bora iliyoshika namba moja kwa Afrika, na Ngorongoro ikiwa namba 5.. Masai Mara ya Kenya ni namba 8. Lakini pia Tanzania tuna Mlima Mrefu zaidi Afrika Mlima Kilimanjaro ambao pia ni kivutia kikubwa cha Utalii.. Lakini maajabu ni kwamba Kenya wanakusanya pato kubwa sana kwenye Utalii kuliko Tanzania. Mwaka 2013 pamoja na matukio ya kigaidi Kenya ilitembelewa na watalii million 1.4 wakati Tanzania yenye amani tele ilitembelewa na watalii million 1.04.. Amani wanayoihubiri CCM na vivutio vyetu vya Utalii bado havijatufaidisha chochote.. Pato la Mtanzania kwa mwaka ni Tshs. 1,996,000 na Pato la Mkenya kwa mwaka ni Tshs. 3,176,000.. Pato la nchi (Tanzania) ni Tshs. Trillion 98.36 na Pato la nchi kwa Kenya ni Tshs. Trillion 140.. Tanzania kuna madini ya kila aina, Tanzanite, Dhahabu, Rubi, Uranium, Makaa ya Mawe, Chuma, Kenya hawana madini ya aina yeyote lakini bado wametuzidi pakubwa kwenye pato la Taifa.. Sekta ya madini inachangia 3.3% kwenye pato la taifa kutokana na mikataba mibovu uliyowekwa na viongozi wa CCM.. Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kilikuwa kinazalisha TYRE bora kabisa za kazi. Kilikuwa na Soko kubwa Afrika Mashariki na kati. Gari zote za Tours zinazotembea porini Afrika Mashariki yote na Afrika ya Kati zilikuwa zinafunga TYRE ya GENERAL. Hata wale wapigana vita za msituni huko Kongo na Sudan walikuwa hawaendi kupambana bila kuhakikisha Land Rover yake imefungwa Tyre ya General. Magari ya serikali yote yalikuwa yanafunga Tyre ya General.. Kiwanda kilikuwa kinalipa kodi isiyopungua Billion 100 kila mwaka.. CCM wakafanya hujuma kukiua, zinatolewa subsidy zinaishia kwenye matumbo yao. Wakenya walivyosmart wakaiba ile Technology ya Tyre za General wakafungua kiwanda chao huko kwao kikaitwa YANA Tyre ambaye sasa ndiye Supplier mkubwa wa Tyre Afrika Mashariki na Kati.. Kampeni zinaanza wamejifanya kuifufua General Tyre, Je, wataweza kupambana na Yana Tyres?? Kenyans are always SMART kuliko akili za CCM CCM wanasema hapa ni Kazi tu.. na kwa mwananchi mwenye akili ndogo atawapigia kura. . IT'S HIGH TIME TO OPT FOR CHANGES
0 Toa maoni yako.
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company