CCM INAVYO NGANGANA KUJISAFISHA NA TOPE.



Na Oscar Samba
Sina dhumuni lakubeza jitiada zinazofanya na safu mpya ya uongozi wa chama cha CCM,kupitia mratibu wao mkuu mh Lukuvi na wakina Philipi Mangula za kutangaza kazi za chAma kwenye vyombo vya habari.
Kwanza ningependa kuomba radhi kwa yeyote yule atakaenielewa vibaya kutokana na kauli hii yangu ya kujisafisha na tope, bali endelea kufwatilia kwani tafsiri yake himo ndani.
Hakuna kitu kibaya duniani au popote pale kama kuto kujitambua au KUSHINDWAkusom alama za nyakati kwa hili CCM sichelei kuwaambia ya kwamba wameshindwa.
Badala ya  kujisahihisha wameanza kutumia zaidi ya milioni 500 kwa ajili yakujitangaza au kutangaza yale mambo yaliofanywa na chama hicho kama harakati za kutangaza namna walivyo tekeleza ilani yao ya uchaguzi ya mwaka 2010,wamebuni mpango huwo na vipindi mbalimbali huruka kwenye baadhi nya runinga ikiwemo ya ITV,TBC1 na Star TV,redio na magazeti.
Kwa uchambuzi wangu siamini kama swala hili ni sahihi sana kwani hakuna mtanzania asie jua yatendekayo wala kuyaonaona kwa sababu utekelezaji wake haofanywi hewani au shimoni ama nchi za ngambo la!hasha hutekelezwa peupe.
Hivi ni nani asiona barabara zinavyo jengwa,shule ambazo zimepachikwa majina mengi ikiwemo yebo yebo,voda faster pia jinsi jeshi la polisi linavyo pewa zana ingawa sio za kisasa.
Ama wanadhani ya kwamba ni watanzania wengi au wapo wasiojua kabisa ya kwamba serikali ya CCM haifanyi chochote?
Wamejenga chuo kikuu cha UDOM kupitia mikopo kutoka katika  Mifuko ya hifadhi ya kijamii  pia wanajenga daraja kubwa lile linalotwa la kigamboni.
Kinacho endelea kunishangaza ni hiki,nikitu gani kinacho wafanya waone ya kwamba hiyo bado ni njia sahihi wakati imekuwa ikifanya hivyo kwa kutumia mabilioni ya shilingi wakati wa sherehe mbali mbali ikiwemo zile za uhuru,muungano sabasaba na nanenane.
                   Kilicho sahihi..
Kwa kweli bila unafiki kama kuna njia sahihi ya kufanya kwa wandugu hawa ni sahihisha  ya fwatayo ili kurudisha imani ya watanzania iliokwisha fifia mioyoni mwao na sio kuishia kujitanza.CCM hamna budi kujitambua kwani huwezi kupeleka kari Mahakani eti! kwa kosa la kuacha njia na kugonga au kuua!!!!
Badala yake utamkamata dereva kwa hiyo CCM jisafisheni kwanza…

Watanzania wamechoshwa na vile jinsi CCM inavyozidi kuwakumbatia mafisadi na kuwatukuza huku wakidiriki kuwasafisha tena hata raisi hutekeleza hayo,mfano yupo Lowassa licha ya kutuhumiwa bali hata walipo izikia richi-mound haojulikani,Mwingine ni Hetrwu Chenge alie wahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwenye miaka ya 1970s na hatimae waziri wa miundo mbinu ambae anahusishwa na wizi au rushwa ya fedha za rada iliobatizwa chenchi za rada.
Kama haitoshi kaifadhi fedha lukuki [zaidi ya dola milioni 1 za kimareakani] kwenye kisiwa kimoja kilichopo huko nchini wingereza na alipo hojiwa aliviita ni vijisent kauli inayotiashaka ya kwamba huenda nyuma ya pazia kuna mengi yalio jificha yaani wapo wezi wengi zaidi kama nitakuwa nimeilewa vilivyo.
Serikali ya CCM kupitia sheria ya maadili kwa umma imekataa kuchukuwa atua,sio hao tuu kwani umesahau jinsi walivyo tuchezea mchezo wa kibaba au danganya toto kwa aliekuwa gavana mkuu wa BOT David Bilali kwa kutudanganya ya kwamba amefariki huku tulio wengi tukibaki tukijiuliza ni kwanini mtuhumiwa akauguzwe bila ulinzi,alikofia ni nje ya nchi ni kwa nini mwili wake usingerejeshwa Tanzania kwa ajili ya mazishi,mbona watanzania wakiwemo waandishi wahabari mbaya zaidi hata mke wake hawakuruhusiwa kwenda kwenye mazishi yake?
kwa majibu mepesi yanayotokana na maswali mazito serikali ya CCM eti! Inajibu ya kwamba mwili wake ulivchomwa moto,je, ni sababu zipi zilizomwafanya kutekeleza ujinga huwo je,niutamaduni wa watanzania au wamarekani.?
Katika hili la ufisadi CCM imechemka tena kwa mafuta yake yenyewe, Mh. Nape wapi ile ahadi yako ya kuwachukulia hatua mafisadi wote iliozaa vua kamba.
Watanzania wanazidi kujiuliza sababu za deni lataifa kuendelea kupaa na kufikia sh.trilioni 22 huku serikali ya CCM kupitia mwenyekiti wake Kikweti ikizidi kujigamba tena adharani ya kwamba bado tunakopesheka.Wenye ufahamu hujiuliza ni nani wakuja kubeba zigo hilo la madeni kama sio watz?.
Wale wageni wakisiasa waliamini ya kwamba sakata la rushwa litakwisha na kubaki kuwa historia,hawakujua ya kwamba rushwa ni CCM na CCM ni rushwa.
Fikira hizo ziliwajia mara tu baada ya kutangazwa kwa safumpya ya chama hicho kilicho jitumbukiza kwenye dimbwi la wizi linalotafuna rasilimali za watz,Safu hiyo mpya iliongozwsa na  P.Mangula na wengine huku sura ya Nape Nauye ikijirudia,kwa makusudi kabisa kwani walijua ahadi zao hazitekelezeki siku mmoja baada ya kutangazwa uwepo wao kule mjini Dodoma waliwasili jijini Dar.
Walivuta breki hadi kwenye viwanja vya sabasaba na kuhaidi kuwashuulikia wale wote waliokuwa wakituhumiwa na rushwa hali iliyovuma zaidi punde zilipofanyika chaguzi zao za kuwatafuta wajumbe wa NEC,kama hauamini mtafute Sumae akusimulie.

Toeni majibu ya kuuzwa kwa nyumba za mawaziri na viongozi waidara mbalimbali ngazi ya mikoa na wilaya haliinayo wasababishia wale wanaoteuliwa sasa kusota kwa kuishi maotelini au nje na maeneo yao.
Wapeni watanzania kauli za shida zao  ikiwemo maji yaligeuka na kuwa kama dhahabu kwani yanapo toka tu watu hujazana na kuarifiana kijiji kizima huku wakina mama wakilazimika kuamka usiku wamanane na wengi hubakwa,kwa hayo kweli hata mkitangaza paka uvunguni ninani atakaerudisha imani kwenu.?
Toeni majibu kwa vitendo ambayo yataonesha kweli ni kwajinsi gaini watz wanavyo tarajia kunufaika na rasilimali zao kama vile gesi na madini,mikataba hiyo inatija gaini? au wataendelea kuambiwa wananufaika huku wawekezaji wakitakiwa kujoa mrahaba wakodi ya asilimia 4% tu na mnajipongeza kwa kupanda kutoa 3-4%.
Wananchi mnao haha kuwatangazia wanataka kujua sababu zinazo lifanya jeshi la poli kuwa juu ya sheria kwani hupiga na kuua watu ovyo,na wameanza kujiohusisha na vitendondo vya wizi ikiwemo nyara za serikali.
Mkumbuke hata hao mnao watangazia na kuwatumia yaani wandishi wahabari nao wanahoji au tunahoji kwanini mauaji ya DEVID MWANGOSI,?
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company