Winfred Zaha anatarajiwa
kufanyiwa uchunguzi wa matibabu katika klabu ya Manchester United siku
chache zijazo kabla ya uhamisho wake kukamilika kutoka kwa klabu ya
Cyrstal Palace.
Ripoti zinasema United imelipa kitita cha pauni
milioni 15 kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye
alijiunga na Crystal palace akiwa na umri wa miaka kumi na miwili.Zaha amesaini mkataba wa miaka mitano na Manchester United na anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza na timu ya taifa ya Uingereza mwezi ujao.
Awali kulikuwa na ripoti kuwa Crystal Palace haikuwa na nia ya kumuuza mchezaji huyo lakini, inaonekana kuwa mazungumzo kati ya kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson na wasimamizi wa klabu hiyo yalizaa matunda.
Sir Alex Ferguson alisalia nyuma baada ya kikosi chake kuelekea nchini Qatar kwa mazoezi zaidi, ili kuendeleza mazungumzo kuhusu usajili wa mchezaji huyo.
Kocha huyo pia alikwenda nchini Scotland kutizama mechi ya Celtic, ili kumchunguza mcheza kiungo wa Celtic, kutoka Kenya, Victor Wanyama.
Wanyama amekuwa nyota wa Celtic, katika michuano ya kuwania ko,be la klabu bingwa barani ulaya.
Wakati wa mechi hiyo Wanyama, aliifungia Celtic bao moja na ripoti zinasema kuwa vilabu vingine vikiwemo Arsenal, Tottenham na Liverpool vile vile vinamsaka mchezaji huyo kutok