Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ameapa kuipeleka migogoro yote baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 4 Machi kwenye mfumo wa kimahakama kwa njia za amani, baada ya ombi la Rais Barack Obama wa Marekani, kiliripoti kituo cha Capital FM cha Kenya siku ya Jumatano (tarehe 6 Februari).
Katika ujumbe kwa njia ya video hapo Jumanne, Obama aliwatolea wito Wakenya kufanya uchaguzi wa amani, huru na haki na kuepuka kurejea kwa ghasia zilizofunika uchaguzi wa 2007.
"Chaguo la nani ataiongoza Kenya ni la watu wa Kenya," alisema Obama. "Marekani haimungi mkono mgombea yeyote, lakini tunaunga mkono uchaguzi wa amani na unaoakisi matakwa ya watu."
"Huu ni wakati wa watu wa Kenya kushirikiana badala ya kugawanyika. Mkifanya hivyo, mtauonesha ulimwengu kwamba nyinyi sio watu wa kabila fulani, bali raia wa taifa kubwa na lenye fahari," alisema.
Odinga aliikaribisha hotuba hiyo ya Obama kwa watu wa Kenya. "Ni jambo linaloridhisha kujua kwamba rais (wa Marekani) anakuwa na hamu binafsi kwa uchaguzi ujao wa Kenya na pia anayajua masuala muhimu yanayoendelea," alisema.
"Tunataka uchaguzi ujao uwe huru, wa haki na wa amani ili wale watakaoshinda waonekane wakiakisi matakwa ya kweli ya watu," alisema Odinga. "Wakenya wanataka kushirikiana kama taifa moja na kuwapigia kura viongozi wanaowataka bila vitisho au ghiliba."