WAFANYA BIASHARA WA KWA-MROMBO WAENDELEA KULALAMA.

Wafanyabiashara wa soko la kwa Morombo jijini Arusha walalamikia mazingira magumu ya ufanyaji kazi.

Wakizungumza na mwandishi wetu wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakifanyia biashara zao nje ya eneo la soko hilo wamesema kwamba ukosefu wamiundombinu ya kuzuia jua unawadhalimu watumie miamvuli  ili kujisitiri na jua hali inayo waongezea majukumu.

Lakini wafanyabiashara wengine waliokuwa wakifanya biashara zao ndani ya soko hilo walilalamika kitendo cha wenzao kufanyabiashara zao njee ya soko hali inayowafanya kukosa wateja angali kwamba eneo rasimi ni landani
 "kama unavyo ona mwandishi hapa vizimba viko wazi lakini wenzetu wapo nje na sisi tuliopo hapa ni wale wenye roho ngumu tuliosema tukomae,alisema kijana mmoja ambae hakupenda kutaja jina lake.

Mwandishi wetu alishuhudia vibanda vya ndani ya soko hilo vikiwa viko wazi,lakini vimeezekwa kwa miundombiniu yenye kuzuia jua, jitiada za kuutafuta uongozi wa soko hilo ili jujibu shutuma hizo bado zinaendelea.

  tunaomba radhi kwa kushindwa kuwaqeka picha kwani ni sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company