Balozi za Tanzania zatumia fedha vibaya : Kabwe

Tanzania Parliament Dodoma.Zitto Kabwe mbungewww.hakileo.blogspot.com

menyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema balozi karibu zote za Tanzania zina utumiaji mbaya wa fedha za umma yaani matumizi bila utaratibu kufuatwa.

Ameeleza kwamba tatizo lililopo ni tatizo la kimfumo au kimuundo hususan kwenye wizara ya mambo ya nje na kujikuta mahesabu ya balozi yamekuwa na matatizo.

Kwahiyo anaeleza kuwa kamati yake ilichofanya kwanza imeagiza ukaguzi maalum kwa wizara ya mambo ya nje  ili pia mdhibiti mkuu na mkaguzi wa hesabu za serikali awasilishe kitu kinachoitwa ukaguzi wa mfumo ili kuweza kujua ni nini kamati yake inaweza kufanya  ili wizara ya mambo ya nje isiwe na hoja za ukaguzi nyingi kama ambavyo imetokea hivi sasa .Kusikiliza mahojiano haya bofya.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company