Simba, Yanga baba yao mmoja
kwa mujibu wa mwananchi
Na Calvin Kiwia, Mwananchi
Posted Jumatatu,Agosti12 2013 saa 16:51 PM
Posted Jumatatu,Agosti12 2013 saa 16:51 PM
Kwa ufupi
Sikutaka kuamini moja kwa moja. Nilichukua simu yangu ya kiganjani na kumpigia ili kuthibitisha ninayosikia mitaa kama ni kweli!
Nilipigwa na mshtuko, baada ya kusikia taarifa
zimeenea mitaani kote kuwa ‘kiraka’ Nurdin Bakari aliyeanzia soka lake
timu ya AFC ya Arusha na kuhamia Simba kabla ya kutua Yanga na kudumu
miaka sita ya mafanikio, ameachana na soka la ushindani.
Sikutaka kuamini moja kwa moja. Nilichukua simu yangu ya kiganjani na kumpigia ili kuthibitisha ninayosikia mitaa kama ni kweli!
Jumatatu ya Julai 9, mwaka huu, muda wa saa 2
usiku, nilimpigia simu Nurdin kwa bahati nzuri alipokea simu yangu na
kunikubalia tufanya naye mahojiano na kunieleza anakoishi Tabata kwa
bibi karibia na Rufita.
Nilipofika kwake mfanyakazi wake wa ndani alitoka
na kunifungulia geti nikaingia ndani na kumuona Nurdin akiwa amesimama
kwenye mlango wa nyumba anayoishi akiwa amembeba mwanaye wa kike Salha,
mwenye umri wa mwaka mmoja na kunikaribisha sebuleni kwake.
Nikaingia na kusalimiana naye huku akionyesha
tabasamu la mbali. Mwanaye Salha pia alinisalimia kwa kuweka mkono wake
kichwani kwangu, ambapo alikaa kwenye kochi na mimi nikakaa kwenye kochi
lingine.
Swali la kwanza kwa Nurdin nilimtaka aniweke wazi
kama ni kweli ameamua kuachana na soka la ushindani kama nilivyokuwa
nikisikia stori mitaani.
Nurdin alionyesha uso wa kutabasamu na kunijibu.
“Hizo ni habari zisizokuwa na ukweli wowote ndani yake. Soka ndiyo
maisha na kazi yangu,” anasema Nurdin huku akiwa anamtizama mwanaye,
Salha aliyembeba.
KUACHWA YANGA
Nurdin anasema amemaliza mkataba wake Yanga na
hakuna anachoidai zaidi ya fedha za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara msimu uliopita.
“Binafsi bado najiamini nina kiwango bora cha
kuendelea kuichezea Yanga, lakini chuki binafsi za viongozi zimefanya
nishindwe kuongezewa mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo,”
Nurdin anasema viongozi walimjengea zengwe na kumchukia baada ya kuwa mstari wa mbele kudai haki yake.
“Kama unataka kuchukiwa na viongozi wa Simba na
Yanga dai haki yako. Utapigwa zengwe hadi utaachwa,” anasema Nurdin
ambaye ambaye amejiungana Rhino Rangers ya Tabora.