Kuna uwezekano Arafat aliuawa kwa Sumu

Aliyekuwa kiongozi wa Palestina Yasser Arafat huenda aliuawa kwa sumu kali ya Polinium.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya kisayansi iliyofanywa na wanasayansi nchini Uswizi ambayo shirika la bahari la Al Jazeera limeweza kupata.


Hata hivyo ripoti za awali kulingana na rekodi za kimatatibu zake hayati Arafat zinasema kuwa alifariki kutokana na kiharusi , kilichosababishwa na ugonjwa wa damu.

Lakini mwili wake ulifukuliwa mwaka jana kwa uchunguzi zaidi kutokana na madai kuwa Arafat aliuawa.
Ripoti hiyo ya wanasayansi kutoka Uswizi, inasema kuwa mwili wa Arafat ulionyesha dalili za kuwa na kiwango kikubwa cha sumu ya Polonium, na hivyo kuunga mkono dhana ya kuuawa kwake kwa sumu.

Wapelestina wengi wameamini kwa miaka mingi kuwa Israel ndio ilimuua Aarafat kwa sumu. Wengine wanadai kuwa alifariki kutokana na ugonjwa wa Ukimwi au Saratani.

Israel imekuwa ikikana madai ya kuhusika na mauaji ya hayati Arafat.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Israel, amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na wanasayansi wa Uswizi ni kama mchezo wa kuigiza tu.

Wanasayansi hao walifanyia uchunguzi wa kina nyaraka za kimatibabu za Arafat, wakachunguza mabakai yake pamoja na vitu alivyokwenda navyo hospitalini mjini Paris kutafuta matibabu alipofariki mwaka 2004.

Walifanyia uchunguzi mifupa yake pamoja na mchanga katika sehemu alikozikwa Arafat.

Wanasayansi hao walisema kuwa matokeo ya utafiti wao yanawiana na madai ya Arafat kuuawa kwa sumu aina ya Polonium-210.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company