Rais Kikwete asema Tanzania kamwe haitajitoa katika Jumuia ya Afrika Mashariki .

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania (kulia) na Rais Joseph Kabila wa DRC (kushoto) wakiingia hotel Hyatt Kilimanjaro.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amelihutubia bunge la nchi hiyo alhamisi likiwa ni jambo la nadra kufanyika akizungumzia masuala mbali mbali ya kitaifa na masuala ya kikanda. Akilihutubia bunge hilo mjini Dodoma Tanzania Rais Kikwete amesisitiza bayana kwamba Tanzania kamwe haitajitoa kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki kwa kuwa ndiyo iliyoianzisha na kuilea kwa lengo la kuleta ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama.
“ Wenzetu wanakutana wanaunda kamati ya ufundi ya technical, kamati ya mawaziri watoe mapendekezo na rasimu ya katiba , kwa kweli unajiuliza maswali mengi mpaka unakosa majibu. Je wenzetu hawa, wamekosa imani na jumuiya wanataka kuunda yao au wanaichukia nchi yetu na hivyo wameamua kutufanyia vitimbi tutoke au sijui wana chuki na mimi napenda kuwahakikishia waheshimiwa wabunge kuwa hatuna mpango wa kutoka katika Jumuiya”. alisema Kikwete.

Amesema chokochoko zilizoanza kujitokeza kwa sasa zimetokana na msimamo wa Tanzania katika masuala ya ardhi, ajira na kuundwa kwa Shirikisho la Afrika ya Mashariki bila kufuata hatua zinazostahiki.

Amesisitiza msimamo huo sio wa kwake peke wala wa viongozi bali ni wa watanzania walio wengi, ambao wanataka kuona jumuia inaundwa hatua kwa hatua na wala siyo kwa haraka haraka.

Miongoni mwa masuala mengine aliyoyazungumzia ni suala la kati na kuchukua muda pia kueleza hatua ya serikali kusitisha operesheni Tokomeza , majangili, na kuahidi hatua kali zitachukuliwa kwa watendaji waliokiuka taratibu, lakini akawataka wabunge kuwaambia wananchi kuzingatia sheria ya wanyamapori, ili kuondoa migongano isiyo ya lazima.

“ Napenda kuwakumbusha nyinyi watunga sheria kuwa sheria ya hifadhi ya wanyamapori hairuhusu mifugo kuchungwa katika maeneo ya hifadhi maeneo yale wanachungwa wanyampori na mchungaji wake ni Game Scout naomba tuwakumbushe wananchi tunaowaongoza wajiepushe na kufanya hivi ni uvunjifu wa sheria za nchi naomba pia wananchi walemishwe ili wajue kuwa wakifanya hivyo na kukutwa maeneo hayo na mifugo yao kuna adhabu iliyotamakwa kwenye sheria” alisema Kikwete.

Rais, ameweka wazi kuwa lengo la operesheni hiyo ilikuwa ni kuokoa kupotea kwa rasilimali ya tembo nchini, kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company