Waandamanaji wanaoipinga serikali wajitokeza kwa wingi Jumatatu kumtaka waziri mkuu kujiuzu
Waziri mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra ametangaza kwamba analivunja bunge na ataitisha uchaguzi wa mapema , "kwa haraka iwezekanavyo" kufuatia maandamano ya zaidi ya mwezi mmoja mjini Bankok kuipinga serikali yake.
Katika hotuba kwa taifa Jumatatu asubuhi kiongozi huyo alisema atawaachia wananchi kuamua mustakbal wa nchi yao.
Hata hivyo kiongozi wa chama cha upinzani cha Demokratic, Suthep Thaungsuban amesema hatositisha maandamano na wataendelea kuandamana hadi ofisi za Bi. Yingluck. Polisi waliripoti kwamba maelfu kwa maelfu ya watu waliandamana kuelekea makao makuu ya serikali siku ya Jumatatu asubuhi.
Wabunge wa upinzani walijiuzulu Jumapili na kusema hawawezi kufanya kazi na bunge linalopingwa na wananchi. wamesema ingawa ameitisha uchaguzi lakini hawatosita hadi Bi Yingluck ameacha madaraka.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago